REHEMA ni nini.
Rehema ni msamaha mbele ya Mungu wa adhabu ya muda kwa
ajili ya dhambi ambazo kosa lao limekwishafutwa, msamaha ambao Mkristo
mwamini aliyejiweka vizuri huupata kwa masharti fulani yaliyopangwa kwa
tendo la Kanisa ambao likawa mgawaji wa ukombozi hutumia mamlaka yake
hazina ya malipizi ya Kristo na ya Watakatifu.
Rehema inaweza kuwa ya muda au kamili kwamba yaondoa au
sehemu au adhabu yote kabisa ya muda inayotakiwa kwa sababu ya dhambi.
Kila muumini anaweza kupata rehema kwa ajili yake au kwa ajili ya
marehemu. (Rej. KWA 1471)
Katika mwaka huu huruma na rehema ya Mungu ni kwa wote wenye nia ya kuipokea rehema ya Mungu katika ukamilifu wake.
Kila mmoja akutane na uso wa huruma ya Mungu anayesamehe bila masharti.
Masharti ya kupata rehema kamili ni:-
Kwa wagonjwa wasioweza kwenda katika hija itoshe kutafakari
Fumbo la Pasaka, kushiriki adhimisho la Misa hata kupitia media hilo ni
hitaji la kuwapatia rehema.
Post a Comment