Barua
ya Upendo wa Baba toka kwa Mungu Baba.
Mwanagu,
Huenda hunijui, lakini najua kila kitu kuhusu wewe,….Zab.139:1. Najua kuketi kwako na kusimama kwako….Zab.139:2. Natambua njia zako zote .Zab.139:3. Hata nywele za kichwa chako zimehesabiwa zote….Mt.10:29 –31. Kwa kuwa umeumbwa kwa sura na mfano wangu….Mwa.1:27. Ndani yangu unaishi, unajimudu na uko, Kwa kuwa wewe ni mtoto wangu ….Mdo.17:28. Nilikujua hata kabla ya kuchukuliwa mimba ….Yer.1:4 – 5. Nilikuteua uwe mwanangu hata kabla ya ulimwengu huu kuumbwa……Efe.1:4. Hukufanyika kwa makosa Zab.139:15 –16. Siku zako zote niliziandika kitabuni mwangu ….Zab.139:15 –16. Nilipanga na kuamua lini uzaliwe na mahali gani uishi ….Mdo.17:26. Umeumbwa kwa namna ya kutisha na ya ajabu …Zab.139:14. Nilikuumba na kukutengeneza mwili wako wote tumboni mwa mama yako ….Zab.139:13. Nimekutegemeza tangu kuzaliwa kwako ….Zab.71:6. Wale mawakala wa uongo wamenitambulisha vibaya kwako kwa sababu wao wenyewe hawanijui … Yoh.8:41 – 44. Pamoja na yote sipo mbali wala hasira nawe, bali mimi ni ukamilifu wa upendo …. 1Yoh.4:16. Na ni hamu yangu kukuza upendo wangu kwako …. 1Yoh.3:1. Basi tu kwa sababu wewe ni mwanangu nami ni Baba yako ….. 1Yoh.3:1. Ninakupatia mema mengi kuliko vile ambavyo baba yako wa duniani angekupatia …. Mt.7:11. Kwa kuwa mimi ni Baba mkamilifu ….. Mt.5:48. Kila kipaji na yote mema upokeayo mikononi mwako yatoka mikononi mwangu …. Yak.1:17. Kwa kuwa mimi ni mfadhili wako na ninajali mahitaji yako yote …. Mt.6:31 –33. Nimekupangia yote mema ili uwe na tumaini la baadaye …. Yer.29 :11. Kwa kuwa nimekupenda kwa mapendo ya daima na kuendelea kuwa mwaminifu kwako …. Yer.31:3. Mawazo yangu ni makuu mno kwako hayawezi kuhesabika, kuliko mchanga wa pwani ya baahari ….Zab.139:17 – 18. Nakufurahia kwa furaha kuu ….Sefania 3:17. Sitaacha kamwe kukutendea mema …Yer.32:40. Wewe ni mteule wangu …Kut.19:5. Nataraji kukutendea mema kwa moyo wangu wote na uchaji wa nafsi yangu yote ….Yer.32:41. Nataka kukuonyesha mambo makubwa yaliyofichika ….Yer.33:3.Ukinitafuta kwa moyo wako wote, utanipata …. Kumb.4:29. Kwa kuwa mimi ndiye nikufundishaye njia zangu kwa faida yako mwenyewe ….Isaya 48:17. Nachohitaji kwako tu ni utii ili nikutiririshie Baraka na kukupatia fanaka katika mambo yako …Isaya 48:18. Hata hivyo kwa kuwa nakupenda mno sipendi kukulazimisha yale usiyoyapenda usije ukajiona wewe ni mtumwa wangu ndiyo maana nimekupa uchaguzi bado wa kuchagua Baraka au laana, uzima au mauti …. Kumb.30:19. Itafute furaha yako kwangu nami nitakujalia unayoyatamani moyoni …. Zab.37:4. Kwa kuwa nafanya kazi daima ndani yako, na kukupa uwezo wa kutaka na kutekeleza mambo yanayopatana na mpango wangu mwenyewe ….. Fil.2:13. Naweza kuwatendea mengi makubwa zaidi ya yale uwezayo kuomba au kufikiria …. Efe.3:20. Kwa kuwa mimi ndiye nikupaye tumaini jema ….1Thes.2:16 – 17. Mimi pia ni Baba ninayekufariji katika taabu zako zote …. 2Kor.1:3 – 4. Ukivunjika moyo au kukata tamaa, nipo karibu nawe …. Zab.34:18. Kama mchungaji abebavyo kondoo, nimekubeba kifuani karibu na moyo wangu …. Isaya 40:11. Siku moja nitafuta machozi yako yote machoni mwako …. Ufu.21:3 – 4. Na kukuondolea uchungu wote ulioteseka nao katika dunia hii ….Ufunuo.21:4. Mimi ni Baba yako na nakupenda kama vile navyompenda mwanangu Yesu …. Yoh.17:23. Sababu kwa Yesu Upendo wangu umedhihirishwa …. Yoh.17:26. Yeye ni mng’ao wa utukufu na mfano kamili wa hali yangu … Ebr.1:3. Na alikuja kukuonyesha kuwa nipo upande wako na sipo kinyume nawe ….Rum.8:31. Na kuwaeleza kuwa sizihesabu dhambi zenu …. 2Kor.5:18 – 19. Yesu alikufa ili wewe nami tupatanishwe …. 2Kor.15:18 –19. Kifo chake ni udhibitisho wa Upendo wangu kwako kuwa mimi ndiye niliyeanza kukupenda kwanza, na si kwamba ulinifanyia chochote chema ili kuvuta upendo wangu kwako …. 1Yoh.4:10. Nilitoa kila kitu nilichopenda ili niweze tena kupata upendo wako ….Rum.8:32. Ukimpokea huyu aliyezawadi kwako, mwanangu Yesu, umenipokea mimi …. 1Yoh.2:23. Na hakuna kitakachokutenganisha na upendo wangu tena …. Rum.8:38 – 39. Rudi uje nyumbani na nitakufanyia sherehe kubwa zaidi ambayo haijapata kushuhudiwa Mbinguni ……Lk.15:7. Nimekuwa Baba siku zote na nitaendelea kuwa Baba ….. Efeso 3:14 – 15. Swali langu ni ….. Utakubali kuwa mwanangu? …….Yoh.1:12 – 13. Ninakusubiri ……Lk.15:11 – 32.
Nakupenda ,
Baba
yako ,
Post a Comment