Kwaya ya Mt. Kizito ya Parokia ya Olosipa, mnamo Jumamosi iliyopita ya tarehe 28-06-2014, waliweza kurekodi nyimbo za dini kwenye Studio za Radio Habari Maalum, Ngaramtoni.  Hii ni Albamu yao ya pili baaada ya ile ambayo inaitwa "UMOJA NA UPENDO", albamu ambayo niya Video inayotamba sana katika soko.

Baadhi ya nyimbo ziizomo kwenye Albam hiyo mpya ni Ee YESU wangu, Ghadhabu ya Bahari, na Acheni MUNGU aitwe MUNGU. Kwa sasa baada ya kurekodi "Audio", wanakwaya hao wako katika mchakato wa kutoa mkanda wa video kutokana na nyimbo hiza walizozirekodi.
Katibu wa Kwaya hiyo Ndugu Upendo Materu amesema kwamba nyimbo walizozirekodi ni nyimbo zenye kumfanya msikilizaji kuzama katika tafakari nzito ambayo inaweza kumfanya kuona ni wapi alipotoka, alipo na anakokwenda katika maisha yake ya kiroho na kuanza kuchukua hatua ya uongofu na kumsifu MUNGU kwa matendoyake mema.

Wanatarajia kuzindua Albamu hiyo ya Video mwanzoni mwa mwezi wa tisa.  Wanawaomba watu wote wenye mapenzi mema kuwaombea ili yote yawe ni kwa sifa na utukufu wake MUNGU na wanadamu wapate wokovu kwa njia ya Kristo Bwana wetu.  Amina.
Baadhi ya Viongozi wa Kwaya ya Mt. Kizito


Post a Comment

 
Top