Kalenda ya mwaka 2014



JANUARI, 2014
05 Januari, 2014: Epifania: (I. Isa. 60:1-6; II. Efe. 3:2-3,5-6; III. Mt. 2:1-12)
·         Utegemezaji Jumuiya ya Mt. Monika
·         Mchango wa pili kwa ajili ya Seminari ya Jimbo
12 Januari, 2014: Ubatizo wa BWANA (I. Isa. 42:1-4,6-7; Mdo. 10:34-38; Mt. 3:13-17)
·         Utegemezaji Jumuiya ya Mt. Veronika
19 Januari, 2014: Dom. Ya 2 ya Mwaka A (I. Isa. 49:3,5-6; II. 1Kor. 1:1-3; III. Yn. 1:29-34)
·         Utegemezaji Jumuiya ya Mt. Yohani Mbatizaji
26 Januari, 2014: Dom ya 3 ya Mwaka A (I. Isa. 9:1-4; II. 1Kor. 1:10-13,17; III. Mt. 4:12-23)
·         Utegemezaji Jumuiya ya Mt. Inyasi wa Loyola
·         Siku ya kuwasilisha mchango kwa ajili ya usafi wa Kanisa toka kila Jumuiya

FEBRUARI, 2014
02 Februari, 2014: Kutolewa BWANA Hekaluni (Mal. 3:1-4; II. Ebr. 2:14-18; III. Lk. 2:22-40)
·         Utegemezaji Jumuiya ya Wat. Yohakimu na Anna
·         Sadaka ya Shukrani Kwa kumaliza mwezi wa Kwanza
06 Februari, 2014: Alhamisi ya kwanza ya mwezi
·         Kuabudu Ekaristi Takatifu kwa kimya kuanzia saa 1:00 asubuhi baada ya misa na kuhitimishwa kwa Masifu ya Jioni na Baraka ya Sakramenti Kuu saa 11:00 kamili.
09 Februari, 2014:Dom. ya 5 ya Mwaka A (I. Isa. 58:7-10; II. 1Kor. 2:1-5; III. Mt. 5:13-16)
·         Utegemezaji Jumuiya ya Mt. Yosefu Mfanyakazi
·         Mchango wa pili kwa ajili ya Seminari ya Jimbo
16 Februari, 2014: Dom. ya 6 ya Mwaka A (I. Ybs. 15:15-20; II. 1 Kor. 2:6-10; III. Mt. 5:17-37)
·         Utegemezaji Jumuiya yaWat. Malaika Wakuu
21 Februari, 2014: Bishop Denis Durning Memorial Fund
·         Misa ya kumwombea Marehemu Askofu Denis Durning- Ngarenaro, saa 10:00 jioni.  Na kupeleka mchango kwa ajili ya Mfuko wa Askofu Denis
23 Februari, 2014: Dom. ya 7 ya Mwaka A (I. Law. 19:1-2,17-18; II. 1Kor. 3:16-23; III. Mt. 5:38-48)
·         Utegemezaji Wanaume wote
·         Siku ya kuwasilisha mchango kwa ajili ya usafi wa Kanisa toka kila Jumuiya
26 Februari, 2014:  Jumatano
·         Mafundisho saa 11:00 kwa wazazi / walezi na wasimamizi wa watoto watakaobatizwa

MACHI, 2014
01 Machi, 2014: Jumamosi
·         Ubatizo wa Watoto wachanga saa 3:00 asubuhi
02 Machi, 2014: Dom. ya 8 ya Mwaka A (I. Isa. 49:14-15; II.  1Kor. 4:1-5;III. Mt. 6:24-34)
·         Utegemezaji Wanawake wote
·         Sadaka ya Shukrani Kwa kumaliza mwezi wa Pili
05 Machi, 2014: Jumatano ya Majivu (I. Yoe. 2:12-18; II. 2 Kor. 5:20-6:2; III. Mt. 6:1-6, 16-18)
·         Mwanzo wa Kipindi cha Kwaresma nan i siku ya lazima kufunga.  Amri ya Kanisa.  Misa ni mbili.  Misa ya kwanza saa 12:30 na misa ya pili saa 11:00 jioni. Kwa kila misa majivu yatabarikiwa na waamini kupakwa.
06 Machi, 2014: Alhamisi ya kwanza ya mwezi
·         Kuabudu Ekaristi Takatifu kwa kimya kuanzia saa 1:00 asubuhi baada ya misa na kuhitimishwa kwa Masifu ya Jioni na Baraka ya Sakramenti Kuu saa 11:00 kamili.
09 Machi, 2014: Dom. ya 1 ya Kwaresima Mwaka A (I. Mwa. 2:7-9, 3:1-7; II. Rum. 5:12-19; III. Mt. 4:1-11)
·         Utegemezaji Jumuiya ya Wat. Petro na Paulo Mitume
·         Mchango wa pili kwa ajili ya Seminari ya Jimbo
12 Machi, 2014: Jumatano
·         Mkutano wa Udekano wa Monduli – Monduli chini
16 Machi, 2014: Dom. ya 2 ya Kwaresima Mwaka A (I. Mwa. 12:1-4a; II2 Tim. 1:8b-10; III. Mt. 17:1-9)
·         Mchango wa pili kwa ajili ya Afya ya mapadre
·         Utegemezaji Jumuiya ya Mt. Fransisko wa Asizi
·         Semina ya Kiroho kwa waamini wote na Pd. Atilio Mnyenyelwa.
17 Machi, 2014:  Jumatatu
·         Semina ya kiroho itaendelea kila siku hadi siku ya Jumamosi kuanzia saa 10:00 hadi saa 12:30 jioni.  Semina itatolewa na Pd. Atilio Mnyenyelwa toka Jimbo Katoliki Dodoma.
21 Machi, 2014: Ijumaa
·         Mkesha wa Kuabudu Ekaristi Takatifu kwa wanakwaya wote wa Ekaristi Takatifu na waamini wote wenye mapenzi mema.  Mkesha utaanza saa 2:30 usiku.
23 Machi, 2014: Dom. ya 3 ya Kwaresima Mwaka A (I. Kut. 17:3-7; II. Rum. 5:1-2, 5-8; III. Yn. 4:5-42)
·         Utegemezaji Jumuiya ya Mt. Teresia wa Mtoto YESU

APRILI, 2014
03 Aprili, 2014: Alhamsi ya kwanza ya mwezi
·         Kuabudu Ekaristi Takatifu kwa kimya kuanzia saa 1:00 asubuhi baada ya misa na kuhitimishwa kwa Masifu ya Jioni na Baraka ya Sakramenti Kuu saa 11:00 kamili.
06 Aprili, 2014: Dom. ya 5 ya Kwaresima Mwaka A (IEze. 37:12-14; II. Rum. 8:8-11; III.  Yn. 11:1-45)
·         Utegemezaji Wanawake wote
·         Sadaka ya Shukrani Kwa kumaliza mwezi wa Machi
·         Wanakwaya wa Kwaya ya Ekaristi kutembelea watoto yatima Kisongo Kanani.
09 Aprili, 2014: Jumatano
·         Mafungo kwa mapadre wote - Burka
10 Aprili, 2014: Alhamisi
·         Hija Kanani mapadre wote kasha Misa ya kubariki Mafuta Matakatifu - Burka
11 Aprili, 2014: Ijumaa
·         Semina kwa Viongozi wote wa Mitaa saa 10:00 jioni
12 Aprili, 2014: Jumamosi
·         Kikao cha Kamati ya Fedha, Uchumi na Mipango saa 11:00.
·         Uchaguzi wa viongozi wa Shirikisho la Vyama vya Kitume Parokiani, saa 11:00 jioni.
13 Aprili, 2014: Dom. ya Matawi ( “Baada ya kubariki matawi kwa maji ya Baraka husomwa Injili ifuatayo: Mt. 21:1-11; I. Isa.. 50:4-7; II. Fip. 2:6-11; III. Mt. 26:14-27:66)
·         Mchango wa pili kwa ajili ya utume wa Vijana Jimbo
·         Utegemezaji Jumuiya ya Mt. Baltazari
·         Semina kwa watoto wote kuanzia saa 9:00 alasiri hadi saa 11:00 jioni
·         Uchaguzi wa Viongozi wa Shirikisho la Kwaya za Parokia (SHIKWAKA) saa 10:00 jioni.

15 Aprili, 2014:  Jumanne
·         Maungamo kwa watoto wote kwa ajili ya kujiandaa na Sikukuu ya Pasaka.  Saa 10:00 jioni.
16 Aprili, 2014: Jumatano
·         Maungamo kwa watu wazima wote kwa ajili ya kujiandaa na Sikukuu ya Pasaka.  Saa 11:00 jioni.
17 Aprili, 2014:  Alhamisi Kuu (I. Kut. 12:1-8, 11-14; II. 1 Kor. 11:23-26; III. Yn. 13:1-15)
·         Misa ya Karamu ya BWANA itaanza saa 11 jioni na kufuatiwa na kuabudu Ekaristi Takatifu hadi saa 6:00 kamili usiku.
Utaratibu wa Kuabudu Ekaristi Takatifu
·         Saa 1 hadi saa 2 ni Jumuiya za Mtaa wa Bethlehemu
·         Saa 2 hadi saa 3 ni Jummuiya za Mtaa wa Yerusalemu
·         Saa 4 hadi saa 5 ni Jumuiya za Mtaa wa Nazareti
·         Saa 5 hadi saa 6 ni Jumuiya za Mtaa wa Galilaya
18 Aprili, 2014:  Ijumaa Kuu (I. Isa. 52:13-53:12; II. Ebr. 4:14-16; 5:7-9; III. Yn. 18:1-19:42)
·         Adhimisho la Mateso ya BWANA litaanza saa 9:00 kamili alasiri likitanguliwa na Ibada ya Njia ya Msalaba.
·         Mchango kwa ajili ya Nchi Takatifu
·         Mwanzo wa Novena ya Huruma ya MUNGU. Itasaliwa baada ya Njia ya Msalaba kabla ya Adhimisho la Mateso ya BWANA.
19 Aprili, 2014:  Jumamosi Kuu (IMwa. 1:1-2:2; II. Mwa 22:1-18; III. Kut. 14:15-15:1; IV. Isa. 54: 5-14; V. Isa. 55:5-14; VI. Bar. 3:9-15,32-4:4; VII. Eze. 36:16-28; VIII. Rum: 6:3-11; IX. Mt. 28:1-10)
·         Adhimisho la Mkesha wa Pasaka litaanza saa 2:00 usiku
·         Waamini walete sehemu ya vyakula watakavyotumia Sikukuu ya pasaka kwa Baraka maalumu.  Vitu kama vile mchele, mkate, unga, mafuta, mayai n.k.
·         Waamini wafike pia na mishumaa.
·         Novena ya Huruma ya MUNGU itasaliwa kwenye Jumuiya Ndogo ndogo
20 Aprili, 2014: Dominika ya Pasaka (I. Mdo. 10:34, 37-43; II. 2 Koi. 3:1-4; III. Yn. 20:1-9)
·         Sikukuu ya Pasaka
·         Utegemezaji Jumuiya ya Mt. Agustino
·         Mchango wa pili kwa ajili ya Seminari ya Jimbo
·         Ibada ya kuwakaribisha wageni waliojiunga na Parokia
·         Novena ya Huruma ya MUNGU itasaliwa kabla ya kumaliza ibada.
21 Aprili, 2014: Jumatatu
·         Novena ya Huruma ya MUNGU itasaliwa kwenye misa ya asubuhi
·         Kikao cha Kamati ya Liturujia na Katekesi.  Saa 11:00 jioni.
22 April, 2014: Jumanne
·         Novena ya Huruma ya MUNGU itasaliwa kwenye misa ya asubuhi
·         Kikao cha Walezi wa Watoto. Saa 11:00 jioni.
23 Aprili, 2014: Jumatano
·         Mafundisho saa 11:00 kwa wazazi / walezi na wasimamizi wa watoto watakaobatizwa
·         Novena ya Huruma ya MUNGU itasaliwa kwenye misa ya asubuhi
·         Kikao cha Kamati ya Haki na Amani.  Saa 11:00 jioni
24 Aprili, 2014: Alhamisi
·         Novena ya Huruma ya MUNGU itasaliwa kwenye misa ya asubuhi
25 Aprili, 2014: Ijumaa
·         Novena ya Huruma ya MUNGU itasaliwa kwenye misa ya asubuhi
·         Kikao cha Kamati ya WAWATA. Saa 11:00 Jioni.
26 Aprili, 2014: Jumamosi
·         Ubatizo wa Watoto wachanga saa 3:00 asubuhi
·         Novena ya Huruma ya MUNGU itasaliwa kwenye misa ya asubuhi
·         Misa ya Somo wa Jumuiya ya Mwenye Heri Papa Yohani Paulo II saa 11:00 jioni
27 Aprili, 2014: Dom. ya 2 ya Pasaka (I. Mdo. 2:42-47; II. 1 Pet. 1:3-9; III. Yn. 20:19-31)
·         Sikukuu ya Huruma ya MUNGU (Waamini wanaalikwa kutoa matoleo maalumu ya kusaidia masikini kama vile fedha, nguo, vyakula n.k)
·         Siku ya kutangazwa Watakatifu Mwenye Heri Papa Yohani Paulo II na Papa Pius wa 12
·         Siku ya Uzinduzi wa Jumuiya teule ya Mt. Yohane Paulo II
·         Utegemezaji Wanaume wote
·         Siku ya kuwasilisha mchango kwa ajili ya usafi wa Kanisa toka kila Jumuiya
·         Mkutano wa Halmashauri ya Parokia mata ru baada ya misa ya kwanza.  Misa itakuwa moja.
·         Kikao cha Kamati Tendaji baada ya Misa ya Kwanza.
28 Aprili, 2014: Junatatu
·         Kikao cha Kamati ya Vijana na Miito. Saa 11:00 Jioni.

29 Aprili, 2014: Jumanne
·         Kikao cha Kamati ya Wasiojiweza. Saa 11:00 Jioni.
30 Aprili, 2014: Jumatano
·         Kikao cha UMAWATA
·         Misa ya Somo wa Jumuiya ya Yosefu Mfanyakazi saa 11:00 (Misa ya kesha)

MEI, 2014
01 Mei, 2014: Alhamisi ya kwanza ya mwezi
·         Sikukuu ya Mt. Yosefu Mfanyakazi.  Misa saa 1:00 asubuhi.  Waamini walete vifaa vyao mbalimbali kwa ajili ya Baraka.
·         Kuabudu Ekaristi Takatifu kwa kimya kuanzia saa 1:00 asubuhi baada ya misa na kuhitimishwa kwa Masifu ya Jioni na Baraka ya Sakramenti Kuu saa 11:00 kamili.
04 Mei, 2014: Dom. ya 3 ya Pasaka: (I. Mdo. 2:14, 22-28; II. 1 Pet. 1:17-21; III. Lk. 24:13-35)
·         Utegemezaji Wanawake wote
·         Sadaka ya Shukrani Kwa kumaliza mwezi wa Nne
·         Kikao cha Kamati ya Fedha, Uchumi na Mipango mara tu baada ya misa ya kwanza.
05 Mei, 2014: Jumatatu
·         Misa katika Jumuiya ya Mt. Monika, saa 11:00 jioni.
06 Mei, 2014: Jumanne
·         Misa katika Jumuiya ya Mt. Klara, saa 11:00 jioni.
07 Mei, 2014: Jumatano
·         Misa katika Jumuiya ya Mt. Baltazari, saa 11:00 jioni.
08 Mei, 2014: Alhamisi
·         Misa katika Jumuiya ya Watakatifu Malaika wakuu, saa 11:00 jioni.
09 Mei, 2014: Ijumaa
·         Misa katika Jumuiya ya Watakatifu Yohakimu na Anna, saa 11:00 jioni.
10 Mei, 2014: Jumamosi
·         Misa katika Jumuiya ya Mt. Inyasi wa Loyola, saa 12:30 asubuhi.
·         Misa katika Jumuiya ya Mt. Antoni wa Padua, saa 11:00 jioni.
11 Mei, 2014: Dom. ya 4 ya Pasaka: (I. Mdo. 2:14a, 36-41; II. 1 Pet. 2:2b-25; IIIYn. 10:1-10)
·         Mchango wa pili kwa ajili ya Miito
·         Utegemezaji Jumuiya ya Mt. Klara wa Asizi
12 Mei, 2014: Jumatatu
·         Misa katika Jumuiya ya Mt. Yosefu Mfanyakazi, saa 11:00 jioni.
13 Mei, 2014: Jumanne
·         Misa katika Jumuiya ya Mt. Veronika, saa 11:00 jioni.
14 Mei, 2014: Jumatano
·         Misa katika Jumuiya ya Mt. Josephine Bhakita, saa 11:00 jioni.
15 Mei, 2014: Alhamisi
·         Misa katika Jumuiya ya Watakatifu Malaika Walinzi, saa 11:00 jioni.
16 Mei, 2014: Ijumaa
·         Misa katika Jumuiya ya Watakatifu Petro na Paulo Mitume, saa 11:00 jioni.
17 Mei, 2014: Jumamosi
·         Misa katika Jumuiya ya Mt. Yuda Tadei, saa 12:30 asubuhi.
·         Baraka kwa wamama wajawazito kwa ajili ya kuwaombea wajifungue salama saa 4:00 asubuhi
·         Misa katika Jumuiya ya Mtakatifu Papa Yohani Paulo II,  saa 11: 00 jioni.

18 Mei, 2014: Dom. ya 5 ya Pasaka:  (I.  Mdo. 6:1-7; II. 1 Pet. 2:4-9; III. Yn. 14:1-12)
·         Utegemezaji Jumuiya ya Mt. Sesilia
·         Mchango wa pili kwa ajili ya Seminari ya Jimbo
·         Semina kwa viongozi wote wa Jumuiya, Vyama vya Kitume, Kwaya na wa mitaa, mara tu baada ya misa ya kwanza.
·         Misa kuu ya kiaskofu ya maadhimisho ya uwepo na utendaji wa Radio Maria Tanzania, misa ya nne Kanisa la Mt. Teresia wa Mtoto YESU saa 5:30.
19 Mei,2014: Jumatatu
·         Misa katika Jumuiya ya Moyo Mtakatifu wa YESU, saa 11:00 jioni.
20 Mei, 2014: Jumanne
·         Misa katika Jumuiya ya Mt. Agustino, saa 11:00 jioni.
21 Mei, 2014: Jumatano
·         Misa katika Jumuiya ya Mt. Sesilia, saa 11:00 jioni.
24 Mei, 2014: Jumamosi
·         Semina kwa wanachama wote wa Vyama vya Kitume saa nane mchana hadi saa 12:00 jioni
25 Mei, 2014: Dom. ya 6 ya Pasaka: (I. Mdo 8:5-8, 14-17;  II. 1Pet 3:15-18;   III.    Yn 14:15-21)
·         Utegemezaji Wanaume wote
·         Siku ya kuwasilisha mchango kwa ajili ya usafi wa Kanisa toka kila Jumuiya
·         Kikao cha Kamati Tendaji baada ya Misa ya Kwanza.

JUNI, 2014

01 Juni 2014: Dom. ya Kupaa kwa BWANA (I. Mdo 1:1-11; II. Efe 1:17-23; III.  Mt 28:16-20)
·         Utegemezaji Wanawake wote
·         Sadaka ya Shukrani Kwa kumaliza mwezi wa Tano
·         Kikao cha Kamati ya Fedha, Uchumi na Mipango mara tu baada ya misa ya kwanza.
02 Juni 2014: Jumatatu
·         Misa katika Jumuiya ya Mt. Yohana Mbatizaji saa 11:00 jioni.
03 Juni 2014: Jumanne
·         Misa katika Jumuiya ya Mt. Fransisko wa Asizi, saa 11:00 jioni.

04 Juni, 2014: Jumatano
·         Mafundisho saa 11:00 kwa wazazi / walezi na wasimamizi wa watoto watakaobatizwa
05 Juni, 2014: Alhamisi ya kwanza ya mwezi
·         Kuabudu Ekaristi Takatifu kwa kimya kuanzia saa 1:00 asubuhi baada ya misa na kuhitimishwa kwa Masifu ya Jioni na Baraka ya Sakramenti Kuu saa 11:00 kamili.
06 Juni, 2014: Ijumaa
·         Misa katika Jumuiya ya Mt. Teresia wa Mtoto YESU, saa 12:30 Asubuhi.

07 Juni 2014: Jumamosi
·         Ubatizo wa Watoto wachanga saa 3:00 asubuhi
08 Juni 2014: Dom. ya Pentekoste (I.  Mdo 2:1-11; II. 1Kor 12:3b-7, 12-13; III. Yn 20:19-23)
·         Mchango wa pili kwa ajili ya utume wa walei
·         Utegemezaji Jumuiya ya Mt. Antoni wa Padua
·         Maonesho ya Vyama vya Kitume parokia
10 Juni 2014: Jumanne
·         Misa katika Jumuiya ya Mt. Benedicto saa 11:00 jioni
13 Juni 2014: Ijumaa
·         Misa ya Sikukuu ya Somo wa Jumuiya ya Mt. Antoni wa Padua
15 Juni 2014: Dom. ya Utatu Mtakatifu: (I. Kut 34:4b-6, 8-9; II. 2Kor 13:11-14; III. Yn 3:16-18)
·         Mchango wa pili kwa ajili ya Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Afrika Mashariki na Kati (CUEA)
·         Utegemezaji Jumuiya ya Mwenye Heri Yohane Paulo wa pili
21 Juni 2014: Jumamosi
·         Baraka kwa wamama wajawazito kwa ajili ya kuwaombea wajifungue salama saa 11:00
22 Juni 2014: Dom. ya Ekaristi Takatifu (I.Kum 8:2-3, 14-16a; II. 1Kor 10:16-17; III. Yn 6:51-58)
·         Utegemezaji Jumuiya ya Mt. Benedicto
·         Mchango wa pili kwa ajili ya Seminari ya Jimbo
·         Maandamano ya Ekaristi Takatifu kwenda katika Parokia ya Ngaramtoni.  Misa ni moja.
24 Juni, 2014: Jumanne
·         Misa ya Somo ya Jumuiya ya Mt. Yohani Mbatizaji saa 11:00 jioni (Misa ya kesha)
27 Juni, 2014: Jumamosi
·         Semina kwa wanakwaya wa kwaya zote, saa 8:00 mchana parokiani.
28 Juni, 2014: Jumamosi
·         Misa ya Somo ya Jumuiy ya Wat. Petro na Paulo Mitume saa 11:00 jioni (Misa ya kesha)
·         Mtihani wa kwanza kwa wanafunzi wa Komunyo ya kwanza saa 8:00 mchana
29 Juni 204: Wat. Petro na Paulo Mitume: (I. Mdo. 12:1-11; II. 2 Tim. 4:6-8, 17-18; III. Mt. 16:13-19)
·         Mchango wa pili kwa ajili ya Mt. Petro
·         Utegemezaji Wanaume wote
·         Siku ya kuwasilisha mchango kwa ajili ya usafi wa Kanisa toka kila Jumuiya
·         Kikao cha Kamati Tendaji baada ya Misa ya Kwanza.

JULAI

03 Julai, 2014: Alhamisi ya kwanza ya mwezi
·         Kuabudu Ekaristi Takatifu kwa kimya kuanzia saa 1:00 asubuhi baada ya misa na kuhitimishwa kwa Masifu ya Jioni na Baraka ya Sakramenti Kuu saa 11:00 kamili.
05 Julai, 2014: Jumamosi
·         Mtihani wa kwanza kwa wanafunzi wa Kipaimara, saa nane mchana
06 Julai 2014: Dom. ya 14 ya Mwaka A (I. Zek 9:9-10; II. Rum 8:9, 11-13;  III. Mt 11:25-30)
·         Utegemezaji Wanawake wote
·         Sadaka ya Shukrani Kwa kumaliza mwezi wa Sita
·         Kikao cha Kamati ya Fedha, Uchumi na Mipango mara tu baada ya misa ya kwanza.
09 Julai, 2014: Jumatano
·         Misa ya Somo wa Jumuiya ya Mt. Veronika saa 11:00
13 Julai 2014: Dom. ya 15 ya Mwaka A (I. Isa 55:10-11; II.Rum 8:18-23; III. Mt 13:1-23)
·         Utegemezaji Jumuiya ya Moyo Mtakatifu wa YESU
·         Mchango wa pili kwa ajili ya Seminari ya Jimbo
·         Sikukuu ya Kwaya ya Ekaristi Takatifu
16 Julai, 2014: Jumatano
·         Mkutano wa Udekano wa Monduli – Moita Bwawani
20 Julai 2014: Dom. ya 16 Mwaka A (I. Hek 12:13, 16-19; II. Rum 8:26-27; III.Mt 13:24-43)
·         Utegemezaji Jumuiya ya Mt. Yuda Tadei
22 Julai,2014: Jumanne
·         Misa ya Somo wa Jumuiya ya Mt. Josefine Bakita saa 11:00 jioni
23 Julai, 2014: Jumatano
·         Misa ya Somo wa Jumuiya ya Baltazari saa 11:00
26 Julai 2014: Jumamosi
·         Misa ya Somo wa Jumuiya ya Watakatifu Yohakimu na Anna saa 11:00
27 Julai 2014: Dom. ya 17 ya Mwaka A (I.1Fal 3:5, 7-12; II. Rum 8:28-30; III. Mt 13:44-52)
·         Utegemezaji Wanaume wote
·         Siku ya kuwasilisha mchango kwa ajili ya usafi wa Kanisa toka kila Jumuiya
·         Kikao cha Kamati Tendaji baada ya Misa ya Kwanza.
31 Julai, 2014: Alhamisi
·         Misa ya Somo wa Jumuiya ya Mt. Inyasi wa Loyola saa 11:00 jioni
03 Agosti 2014: Dom. ya 18 ya Mwaka A (I. Isa 55:1-3; II. Rum 8:35, 37-39; III. Mt 14:13-21)
·         Mchango wa pili kwa ajili ya Mawasiliano
·         Utegemezaji Wanawake wote
·         Kikao cha Kamati ya Fedha, Uchumi na Mipango mara tu baada ya misa ya kwanza.
·         Kuwasilisha Fedha kwa ajili ya Mfuko wa Jimbo
·         Sadaka ya Shukrani Kwa kumaliza mwezi wa Saba
06 Agosti, 2014: Jumatano
·         Mkutano wa UMAWATA - Burka
07 Agosti, 2014: Alhamisi ya kwanza ya mwezi
·         Kuabudu Ekaristi Takatifu kwa kimya kuanzia saa 1:00 asubuhi baada ya misa na kuhitimishwa kwa Masifu ya Jioni na Baraka ya Sakramenti Kuu saa 11:00 kamili.
10 Agosti 2014:  Dom. ya 19 ya Mwaka A (I.1Fal 19:9a,11-13a; II. Rum 9:1-5; III.Mt 14:22-33)
·         Utegemezaji Jumuiya ya Mt. Josephine Bakhita
·         Mchango wa pili kwa ajili ya Seminari ya Jimbo
11 Agosti 2014:  Jumatatu
·         Misa ya somo wa Jumuiya ya Mt. Fransisko wa Asizi
12 Agosti, 2014: Jumanne
·         Semina kwa Viongozi wote wa Mitaa saa 10:00 jioni
16 Agosti 2014: Jumamosi
·         Siku ya wazazi Oldonyosambu Seminari
·         Semina kwa watu wa ndoa na wale wanaotarajia kufunga ndoa, saa 8:00 mchana hadi saa 12:00 jioni.
17 Agosti 2014: Dom. ya 20ya Mwaka A (           I. Isa. 56:1,6-7; II.Rum. 11:13-15,29-32; III.  Mt. 15:21-28)
·         Utegemezaji Jumuiya ya Mt. Monika
·         Semina kwa watu wa ndoa na wale wanaotarajia kufunga ndoa, mara tu baada ya misa ya kwanza.
22 Agosti, 2014: Ijumaa
·         Semina ya Vijana wote Kituo cha Malezi – Usa river.  Kuingia saa 11:00 jioni
23 Agosti, 2014: Jumamosi
·         Semina ya Vijana wote Kituo cha Malezi – Usa river.
·         Ungamo la kwanza kwa wanafunzi wa Komunyo ya kwanza saa 10:00 jioni
24 Agosti 2014: Dom. ya 21 ya Mwaka A (          I. Isa 22:19-23; II. Rum 11:33-36;  III. Mt 16:13-20)
·         Utegemezaji Jumuiya ya Mt. Veronika
·         Semina ya Vijana wote Kituo cha Malezi – Usa river.
27 Agosti, 2014: Jumatano
·         Misa ya Somo wa Jumuiya ya Mt. Monika (Saa 11:00 jioni)
28 Agosti, 2014: Alhamisi
·         Misa ya Somo wa Jumuiya ya Mt. Agustino (Saa 11:00 jioni)
30 Agosti 2014: Jumamosi
·         Kikao cha Kamati Tendaji saa 11:00 jioni.
31 Agosti 2014: Dom. ya 22 ya Mwaka A (          I. Yer 20:7-9; II. Rum 12:1-2; III. Mt 16:21-27)
·         Utegemezaji Wanaume wote
·         Siku ya kuwasilisha mchango kwa ajili ya usafi wa Kanisa toka kila Jumuiya
·         Ibada ya kuwakaribisha wageni waliojiunga na Parokia
·         Mkutano wa Halmashauri ya Parokia mata ru baada ya misa ya kwanza.  Misa itakuwa moja.
03 Septemba, 2014: Jumatano
·         Mafundisho saa 11:00 kwa wazazi / walezi na wasimamizi wa watoto watakaobatizwa
04 Septemba, 2014: Alhamisi ya kwanza ya mwezi
·         Kuabudu Ekaristi Takatifu kwa kimya kuanzia saa 1:00 asubuhi baada ya misa na kuhitimishwa kwa Masifu ya Jioni na Baraka ya Sakramenti Kuu saa 11:00 kamili.
06 Septemba 2014: Jumamosi
·         Ubatizo wa Watoto wachanga saa 3:00 asubuhi
·         Mtihani wa mwisho kwa wanafunzi wa Komunyo ya kwanza saa 8:00 mchana.
·         Kikao cha Kamati ya Fedha, Uchumi na Mipango saa 11.00 jioni.
07 Septemba 2014: Dom. ya 23 ya Mwaka A (I. Eze 33:7-9; II. Rum 13:8-10; III. Mt 18:15-20)
·         Mchango wa pili kwa ajili ya Msamaria Mwema
·         Utegemezaji Wanawake wote
·         Sadaka ya Shukrani Kwa kumaliza mwezi wa Nane
·         Semina kwa viongozi wote wa Jumuiya, Vyama vya Kitume, Kwaya na wa mitaa, mara tu baada ya misa ya kwanza.
·         Semina kwa watoto wote saa 9:00 hadi saa 11:00 jioni
14 Septemba 2014: Dom. ya 24 ya Mwaka A (I.Hes. 21:4-9; II. Fil. 2:6-11; III. Yn. 3:13-17)
·         Utegemezaji Jumuiya ya Mt. Yohani Mbatizaji
·         Mchango wa pili kwa ajili ya Seminari ya Jimbo
·         Wanakwaya wa Kwaya ya Ekaristi Takatifu na watu wote wenye mapenzi mema kutembelea wafungwa
21 Septemba 2014:   Dom. ya 25 ya Mwaka A (I. Isa 55:6-9; II. Flp 1:20-24; III. Mt 20:1-16)
·         Utegemezaji Jumuiya ya Mt. Inyasi wa Loyola
26 Septemba, 2014: Ijumaa
·         Mwanzo wa Novena kwa ajili ya wototo wa komunyo hadi 04-10-2014
27 Septemba, 2014: Jumamosi
·         Baraka kwa wamama wajawazito kwa ajili ya kuwaombea wajifungue salama saa 04:00 asubuhi.
·         Maungamo kwa watoto wa Komunyo ya kwanza kwa ajili ya kurudia ahadi za ubatizo.
·         Mtihani wa mwisho kwa wanafunzi wa Kipaimara, saa 8:00 mchana.
28 Septemba 2014: Dom. ya 26 ya Mwaka A (I.Eze 18:25-28; II. Flp 2:1-11; III. Mt 21:28-32)
·         Utegemezaji Wanaume wote
·         Siku ya kuwasilisha mchango kwa ajili ya usafi wa Kanisa toka kila Jumuiya
·         Ibada ya kurudia ahadi za ubatizo kwa watoto wa Komunyo ya kwanza misa ya kwanza.  Misa itakuwa moja.
·         Kikao cha Kamati Tendaji baada ya Misa ya Kwanza.
·         29 Septemba, 2014: Jumatatu
·         Misa ya Somo wa Jumuiya ya Watakatifu Malaika Wakuu saa 11:00 jioni

OKTOBA
01 Oktoba, 2014: Jumatano
·         Misa ya Somo wa Jumuiya ya Mt. Teresia wa Mtoto YESU saa 11:00 jioni
·         Ungamo la mwisho kwa watoto wa Komunyo ya kwanza saa 10:00 jioni.
02 Oktoba, 2014: Alhamisi ya kwanza ya mwezi
·         Kuabudu Ekaristi Takatifu kwa kimya kuanzia saa 1:00 asubuhi baada ya misa na kuhitimishwa kwa Masifu ya Jioni na Baraka ya Sakramenti Kuu saa 10:00 kamili.
·         Misa ya Somo wa Jumuiya ya Wat. Malaika walinzi saa 11:00 jioni
03 Oktoba, 2014: Ijumaa
·        Ibada ya kubariki mavazi saa 11:00  
04 Oktoba 2014: Jumamosi
·         Misa ya Somo wa Jumuiya ya Mt. Fransisko wa Asizi
5 Oktoba 2014: Dom. ya 27 ya Mwaka A (I. Isa 5:1-7; II.  Flp 4:6-9; III. Mt 21:33-43)
·         Mchango wa pili kwa ajili ya Uinjilishaji
·         Utegemezaji Wanawake wote
·         Sikukuu ya Komunyo ya Kwanza.  Misa itaanza saa 3:00 asubuhi.
·         Sadaka ya Shukrani Kwa kumaliza mwezi wa Kwanza
12 Octoba 2014: Dom. ya 28 ya Mwaka A (I. Isa 25:6-10; II. Flp 4:12-14, 19-20;III. Mt 22:1-14)
·         Mchango wa pili kwa ajili ya AMECEA
·         Utegemezaji Jumuiya ya Wat. Yohakimu na Anna
·         Kikao cha Kamati ya Fedha, Uchumi na Mipango mara tu baada ya misa ya kwanza.
19 Octoba 2014:        Dom. ya 29 ya Mwaka A (I. Isa 45:1, 4-6; II. 1Thes 7:1-5; III. Mt 22:15-21)
·         Mchango wa pili kwa ajili ya misioni
·         Utegemezaji Jumuiya ya Mt. Yosefu Mfanyakazi
·         Mafungo ya Mapadre – Maua, Moshi, hadi tarehe 25-10-2014
23 Oktoba 2014: Alhamisi
·         Mwanzo wa Novena kwa wanafunzi wa Kipaimara.  Novena itakuwa ikisaliwa kila siku kwenye misa za asubuhi hadi tarehe 31-10-2014.
25 Oktoba 2014: Jumamosi
·         Maungamo kwa wanafunzi wa Kipaimara kwa ajili ya matayarisho ya ibada maalumu ya matamanio ya kumpokea ROHO MTAKATIFU, saa 10:00 jioni.
26 Oktoba 2014: Dom. ya 30 ya Mwaka A (I. Kut 22:21-26; II. 1Thes 1:5-10; III. Mt 22:34-40)
·         Utegemezaji Wanaume wote
·         Mchango wa pili kwa ajili ya Seminari ya Jimbo
·         Siku ya kuwasilisha mchango kwa ajili ya usafi wa Kanisa toka kila Jumuiya
·         Kikao cha Kamati Tendaji baada ya Misa ya Kwanza.
·         Ibada ya Matamanio ya kumpokea ROHO MTAKATIFU, misa ya kwanza.
28 Oktoba, 2014: Jumanne
·         Misa ya Somo wa Jumuiya ya Wat. Simoni na Yuda Mitume saa 11:00 jioni
29 Oktoba, 2014: Jumatano
·         Maungamo kwa wanafunzi wa Kipaimara, saa 10:00 jioni.
31 Oktoba, 2014: Ijumaa
·         Ibada ya kubariki mavazi ya wanafunzi wa Kipaimara, saa 11:00 jioni.

NOVEMBA

01 Novemba, 2014: Jumamosi
·         Sikukuu ya Watakatifu wote (I. Ufu. 7:2-4, 9-14; II. 1 Yoh. 3:1-3; Mt. 5:1-12)
·         Misa saa 1:00 asubuhi
·         Kikao cha Kamati ya Fedha, Uchumi na Mipango saa 11.00 jioni.
02 Novemba 2014: Dom. ya Marehemu Wote (I.Hek. 3:1-9; II. Rum. 6:3-9; III. Mt. 31-46)
·         Sikukuu ya Kipaimara
·         Mchango wa pili kwa ajili ya Chama Cha Biblia Tanzania
·         Utegemezaji Wanawake wote
·         Sadaka ya Shukrani Kwa kumaliza mwezi wa Kumi
06 Novemba, 2014: Alhamisi ya kwanza ya mwezi
·         Kuabudu Ekaristi Takatifu kwa kimya kuanzia saa 1:00 asubuhi baada ya misa na kuhitimishwa kwa Masifu ya Jioni na Baraka ya Sakramenti Kuu saa 11:00 kamili.
09 Novemba 2014:   Dom. ya 32 ya Mwaka A (I. Eze. 43:1-2,4-7; II.  1 Kor. 3:9-13, 16-17; III.  Yn. 2:13-22)
·         Mchango wa pili kwa ajili ya CECAM
·         Utegemezaji Jumuiya ya Wat. Malaika wakuu
12 Novemba, 2014: Jumatano
·         Mkutano wa Udekano wa Monduli - Olosipa
15 Novemba, 2014: Jumamosi
·         Semina kwa wanachama wote wa Vyama vya Kitume, saa 8:00 mchana hadi saa 12:00 jioni
16 Novemba 2014: Dom. ya 33 ya Mwaka A (I. Mit 31:10-13, 19-20,30-31; II. 1Thes 5:1-6;     III. Mt 25:14-30)
·         Utegemezaji Jumuiya ya Wat. Petro na Paulo Mitume
·         Mchango wa pili kwa ajili ya Seminari ya Jimbo
·         Semina ya Vijana wote Parokiani mara tu baada ya misa ya kwanza.
·         Semina kwa watoto wote saa 9:00 hadi saa 11:00 jioni
19 Novemba, 2014:  Jumatano
·         Kikao cha UMAWATA - Burka

22 Novemba, 2014 Jumamosi
·         Misa ya Somo wa Jumuiya ya Mt. Sesilia saa 11:00 jioni
23 Novemba 2014: YESU KRISTO MFALME (I. Eze. 34:11-12, 15-17; II. 1Kor. 15:20-26,28; III. Mt. 25:31-46)
·         Utegemezaji Jumuiya ya Mt. Fransisko wa Asizi
·         Semina kwa wanakwaya wa kwaya zote, saa 8:00 mchana parokiani.
·         Kikao cha Kamati Tendaji baada ya Misa ya Kwanza.
29 Novemba, 2014: Jumamosi
·         Semina ya Vijana wote Parokiani saa 8:00 mchana
30 Novemba 2014:    Dom. ya 1 ya Majilio Mwaka B. (I. Isa 63:16-17, 64:1, 4-8; II. 1Kor 1:3-9;  III.  Mk 13:33-37)
·         Utegemezaji Wanaume wote
·         Siku ya kuwasilisha mchango kwa ajili ya usafi wa Kanisa toka kila Jumuiya
·         Kuhamasisha juu ya Sikukuu ya Somo wa Paokia
·         Mkutano wa Halmashauri ya Parokia mata ru baada ya misa ya kwanza.
03 Desemba, 2014: Jumatano
·         Semina kwa Viongozi wote wa Mitaa saa 10:00 jioni
04 Desemba, 2014: Alhamisi ya kwanza ya mwezi
·         Kuabudu Ekaristi Takatifu kwa kimya kuanzia saa 1:00 asubuhi baada ya misa na kuhitimishwa kwa Masifu ya Jioni na Baraka ya Sakramenti Kuu saa 11:00 kamili.
05 Desemba, 2014: Ijumaa
·         Maungamo kwa kujiandaa na Sikukuu ya somo (Watoto saa 9:30; Watuwazima saa 11:00 jioni)
06 Desemba 2014: Jumamosi
·         Kikao cha Kamati ya Fedha, Uchumi na Mipango saa 11:00 jioni.
07 Desemba 2014: Dom. ya 2 ya Majilio Mwaka B. (I. Isa 40:1-5, 9-11; II. 2Pet 3:8-14; III. Mk 1:1-8)
·         Sikukuu ya Somo wa Parokia (Misa itakuwa moja)
·         Ndoa za Jumla na michezo
·         Mchango wa pili kwa ajili ya Utoto Mtakatifu
·         Utegemezaji Wanawake wote
·         Sadaka ya Shukrani Kwa kumaliza mwezi wa Kumi na moja
·         Sikukuu ya Shukrani
13 Desemba, 2014: Jumamosi
·         Semina kwa watu wa ndoa na wale wanaotarajia kufunga ndoa, saa 8:00 mchana hadi saa 12:00 jioni.
14 Desemba 2014: Dom. ya 3 ya Majilio Mwaka B. (I. Isa 61:1-2, 10-11; II. 1Thes 5:16-24; III.  Yn 1:6-8, 19-28)
·         Mchango wa pili kwa ajili ya  Nchi Takatifu
·         Utegemezaji Jumuiya ya Mt. Teresia wa Mtoto YESU
·         Semina kwa watu wa ndoa na wale wanaotarajia kufunga ndoa, mara tu baada ya misa ya kwanza.
·         Wanakwaya wa Kwaya yab Ekaristi Takatifu na watu wote wenye mapenzi mema kutembelea wagonjwa hosipitali ya Mount Meru.  Saa nane mchana.

21 Desemba 2014:  Dom. ya 4 ya Majilio Mwaka B. (I. 2Sam 7:1-5, 8-11, 16; II. Rum 16:25-27; III. Lk 1:26-38)
·         Utegemezaji Jumuiya ya Mt. Baltazari
·         Mchango wa pili kwa ajili ya Seminari ya Jimbo
·         Kikao cha Kamati Tendaji baada ya Misa ya Kwanza.
22 Desemba, 2014: Jumatatu
·         Mafundisho saa 11:00 kwa wazazi / walezi na wasimamizi wa watoto watakaobatizwa
·         Maungamo kwa watoto wote saa 10:00 kamili jioni kwa maandalizi ya Sikukuu ya Noeli.
23 Desemba,2014: Jumanne
·         Maungamo kwa watuwazima wote saa 11:00 kamili jioni kwa maandalizi ya Sikukuu ya Noeli.
25 Desemba, 2014:  Kuzaliwa kwake YESU KRISTO (I. Isa. 52:7-10; II. 2:Ebr. 1:1-6; III. Yn. 1:1-18)
·         Misa zitakuwa mbili kama kawaida.
26 Desemba, 2014: Sikukuu ya Mt. Stefano, Shahidi (I. Mdo. 6:8-10; 7:54-60; II. Mt. 10: 17-22)
·         Misa itakuwa moja saa 1:00 asubuhi
·         Sikukuu ya Wanakwaya wote
27 Desemba 2014: Jumamosi
·         Ubatizo wa Watoto wachanga saa 3:00 asubuhi
·         Baraka kwa wamama wajawazito kwa ajili ya kuwaombea wajifungue salama saa 11:00
28 Desemba 2014: Dom. ya Familia  Takatifu    (I.YbS 3:2-6, 12-14; II. Kol 3:12-21; III.   Lk 2:22-40)
·         Utegemezaji Wanaume
·         Siku ya kuwasilisha mchango kwa ajili ya usafi wa Kanisa toka kila Jumuiya
·         Ibada ya kuwakaribisha wageni waliojiunga na Parokia

31 Desemba 2014: Jumatano
·       Misa ya kufunga mwaka wa 2014 itaanza saa 11:30 Jioni

******************************

Ratiba ya saa za misa siku za wiki
Jumatatu hadi Ijumaa
Misa ya asubuhi saa 12 :30 asubuhi ikitanguliwa na masifu ya asubuhi saa 12 :00 asubuhi

Ratiba ya Saa za misa siku za Dominika
Misa ya kwanza saa 1 :00 asubuhi (Misa kwa ajili ya watu wazima)
Misa ya pili  saa 3 :30 asubuhi (Misa kwa ajili ya Vijana nawatoto)

Ratiba ya Maungamo
Jumamosi saa  1:00 – 2 :00 asubuhi na saa 10:30 hadi saa 12:00 jioni na wakati wowote pale mwamini anapokuwa anahitaji kupokea sakramenti hiyo.
N.b.Sakramenti ya Kitubio yaweza kutolewa saa yeyote panapotokea hitaji.

Ratiba ya Mafundisho
Komunyo ya Kwanza na Kipaimara-
Jumamosi saa 8:00alasiri  hadi saa 11:00 jioni
Jumapili saa 8:00 mchana hadi saa 11:00 jioni

Ibada ya Baraka ya Sakramenti Kuu
            Kila siku ya Alhamisi saa 11:00 jioni.


Ibada ya kuabudu sakramenti Kuu kwa siku nzima
Kila siku ya Alhamisi ya kwanza ya Mwezi kuanzia saa 1:00 asubuhi hadi saa 12:00 jioni.

Baraka mbalimbali zinazoweza kutolewa na Padre kwa waamini wanaohitaji :-
Baraka ya Familia. Baraka ya Watoto. Baraka ya Wachumba. Baraka ya Wazazi kabla ya Mtoto kuzaliwa.Baraka ya Mama kabla na baada ya mtoto kuzaliwa.  Baraka ya Mama ambaye mimba imetoka.  Baraka ya Wazazi wenye mtoto wa kumlea.  Baraka ya Siku ya kuzaliwa. Baraka ya Walimu na wanafunzi.  Baraka ya Wasafiri (Mtu anayetaka kusafiri). Baraka ya Eneo la ujenzi. Baraka ya Ofisi – Duka – Kiwanda. Baraka ya Vyombo vya usafiri. Baraka ya Vyombo vya Kazi. Baraka ya Wanyama. Baraka ya Mashamba.

Vyama vya Kitume
Parokia ina vyama vya kitume vifuatavyo:
1.      Shirika la Mt. Yosefu
Wanachama wake hukutana kila Alhamisi mara tu baada Baraka ya Sakramenti Kuu kwenye Kanisa dogo.

2.      Shirika la Kipapa.
(Utoto wa YESU).  Wanachama hukutana kila siku ya Ijumaa saa 10:00 jioni na Jumamosi saa 10:00 jioni kwenye kanisa dogo.

3.      VIWAWA
Wanachama wake hukutana kila Dominika mara tu baada ya misa ya kwanza.

4.      WAWATA
Wanachama wake hukutana kila Dominika ya mwisho wa mwezi, kanisani.

5.      Kwaya ya Mt. Kizito
Wanakwaya hukutana kwa mazoezi kila siku za Jumanne, Alhamisi na Jumamosi.

6.      Kwaya ya Ekaristi Takatifu
Hukutana kwa mazoezi kila siku za Jumanne, Jumatano, Ijumaa na Jumamosi.

7.      Mt. Aloisi
Wanachama wake hukutana kila siku ya Jumamosi kuanzia saa 8:00 mchana.
8.      Shirika la Mt. Anna
Hukutana kila siku ya Jumamosi Jioni saa 10:00

KAMATI MBALIMBALI
Kamati Tendaji
Inaundwa na:-
Paroko, Mwenyekiti wa Parokia, Makamu Mwenyekiti, Katibu, Katibu Msaidizi, Mweka hazina na (Mweka hazina Msaidizi).

Baraza la kichungaji
Linaundwa na:-
Wajumbe wote wa Kamati Tendaji, Mwenyekiti na Katibu wa kila Mtaa, Mwenyekiti na Katibu wa kila Kamati ndogo ambazo ni:- Kamati ya Liturujia na Katekesi, Kamati ya Fedha na mipango, Kamati ya Watoto, Kamati ya Haki na Amani, Kamati ya WAWATA, Kamati ya Shirikisho la Kwaya, Kamati ya Shirikisho la Vyama vya Kitume, Kamati ya wasiojiweza, Kamati ya Vijana na Miito.

Halmashauri ya Parokia
Inaundwa na:- Viongozi wote wa Jumuiya Ndogo Ndogo, Viongozi wote wa Vyama vya Kitume na wajumbe wa Kamati ya Fedha, uchumi na mipango.

Viongozi wa Mitaa
Viongozi wote wa  Mtaa Mwenyekiti, Katibu na Mweka hazina.

MAJUKUMU YA KAMATI ZA MITAA / KATA NA KAMATI NDOGO NDOGO ZA PAROKIA
MAJUKUMU YA VIONGOZI WA MITAA / KATA

Kuhimiza  uhai wa Jumuiya katika kipindi chote cha utendaji wao.
Kuhakikisha  wajumbe wote 11 kwa kila Jumuiya wapo, na ikiwa pametokea upungufu wa mjumbe yeyote katika wale 11, watoe taarifa kwa Kamati Tendaji ya Parokia ili uchaguzi mdogo ufanyike mara moja.
Waitishe vikao vya pamoja na hao wajumbe 11 wa kila Jumuiya.  Vikao hivyo viitishwe kila baada ya miezi mitatu ili kupata maendeleo ya Jumuiya hizo na kutoa taarifa yao kwa mikutano ya Kamati ya Utekelezaji ya Parokia ambayo inafanya vikao vyake kila baada ya miezi mitatu.
Kutembelea Jumuiya zao mara kwa mara ili kujua matatizo yaliyopo Jumuiyani, na kujaribu kuyatatua.  Kama tatizo ni  kubwa kiasi cha kushindwa kulikabili, watoe taarifa kwa Kamati Tendaji ya Parokia kwa ufumbuzi zaidi.
Kuhimiza  na kuhakikisha wajumbe wote 11 wanaonyesha mifano bora kwenye Jumuiya zao kwa mahudhurio mazuri katika siku maalum walizojipangia kusali.
Wawe wafuatiliaji na wahamasishaji wa utoaji wa michango ya Kanisa, kama:- Zaka, Sadaka, Vipaji na michango mingineyo iliyopitishwa na kukubaliwa na Baraza la Parokia , kushiriki shughuli mbalimbali za Parokia n.k.
Kuhakikisha na kufuatilia  suria na nyumba ndogo vinatoweka kabisa katika mitaa yao, tukianzia na Viongozi.
Kuwahimiza na kuhakikisha viongozi 11 kwa kila Jumuiya  kwamba wanafanya vikao vyao kama ilivyoagizwa kwenye katiba.
Kuhimiza Jumuiya  Ndogo Ndogo kutukuza somo wao kila mwaka kwa adhimisho la Misapamoja na somo wa Mtaa,  na ikiwezekana wafanye sherehe ndogo baada ya maandalizi ya kiroho kama vile kupokea Sakramenti ya Kitubio, au kufanya Novena n.k.
Kuhudhuria vikao vya Baraza la Kicungaji / Halmashauri ya Utekelezaji Parokia.

MAJUKUMU YA KAMATI NDOGO NDOGO ZA PAROKIA

MAJUKUMU YA KAMATI YA LITURUJIA NA KATEKESI
Kupanga na kusimamia shughuli na huduma mbali mbali Kanisani.
Kuhakikisha kwamba Liturujia ya Kanisa kwa mwaka mzima inafuatwa.
Kupendekeza na kuteua wasimamizi Kanisani.
Kuthibiti nidhamu na kero zilizopo Kanisani.
Kuratibu ufundishaji wa sala na ibada Kanisani.
Kusimamia usafi na mapambo Kanisani (mazingira ya ndani na nje).
Kuhakikisha kwamba Kwaya inawashirikisha waamini katika nyimbo za Liturujia.
Kuweka ratiba muhimu za Ibada Kanisani.
Kusimamia na kutunza vifaa vyote vya huduma Kanisani.
Kuratibu na kusimamia mafundisho ya dini shuleni  na vyuo ambavyo viko katika eneo la Parokia.
Kufanya vikao na Semina kuunganisha wawakilishi wa Liturujia na Katekesi kutoka Jumuiya Ndogo Ndogo.
Ufundishaji wa Katekismu na sala Jumuiyani na kwa makundi mbali mbali kwa njia ya Semina.
Kuratibu mafundisho endelevu ya waamini kuhusu Imani, kuanzia Jumuiyani hadi Parokiani.
Kuandaa njia mbali mbali za kueneza Injili. Mfano:- Vipeperushi na michoro mbali mbali, makongamano na mafungo.
Kuweka utaratibu wa Vikao vya Kamati ya Liturujia na Wasimamizi wa Kanisani.
Kuhudhuria vikao vya Baraza la Kichungaji / Halmashauri ya Utekelezaji Parokia.
Mfundisho ya ndoa na watumishi wa Misa.

MAJUKUMU YA KAMATI YA WATOTO
Kuhakikisha watoto wanapatiwa mafundisho msingi ya Imani Katoliki.
Kuratibu na kusimamia malezi ya watoto kuanzia Jumuiyani, hadi Parokiani.
Kusaidiana na Viongozi wa Jumuiya Ndogo Ndogo kuwawezesha watoto kutambua miito yao.
Kufanya vikao na Semina kuunganisha wawakilishi wa Watoto kutoka Jumuiya Ndogo Ndogo.
Kubuni na kuandaa mafundisho, taratibu mbali mbali za michezo, burudani na vivutio mbali mbali kwa watoto vyenye mwelekeo wa kuwafundisha maadili.
Kuhakikisha Watoto wanahudhuria Misa yao kadiri ya ratiba ya Kanisa.  
Kuandaa vikao vya kamati ya Watoto
Kuhudhuria vikao vya Baraza la Kichungaji / Halmashauri ya Utekelezaji Parokia.

MAJUKUMU YA KAMATI YA HAKI NA AMANI
Kuelimisha jamii  ya Parokia yetu kuhusu haki za raia.
Kuhakikisha kuwa Haki na Amani inakuwepo katika familia, Jumuiya hadi Parokia.
Kufanya vikao na Semina kuunganisha wawakilishi wa Haki na Amani kutoka Jumuiya Ndogo Ndogo.
Kuunda Baraza la usuluhishi wa ndoa kulingana na mujibu wa sheria ya nchi.
Kusuluhisha migogoro katika familia za Parokia yetu.
Kubuni mbinu za kuwezesha Haki na Amani kupenyeza katika familia za Parokia yetu.
Kuandaa vikao vya Kamati za Haki na Amani
Kuhudhuria vikao vya Baraza la Kichungaji / Halmashauri ya Utekelezaji Parokia.

MAJUKUMU YA KAMATI YA WAWATA
Kuwasaidia kina mama kuelewa na kutekeleza Utume wao katika Kanisa.
Kuwaelekeza kadiri ya mwongozo wa WAWATA Jimbo, kuelewa na kutimiza vema Katiba ya Wanawake Wakatoliki Tanzania.
Kuwahimiza katika maendeleo yao ya kiroho na kimwili.
Kuwaandalia ratiba ya shughuli za matendo ya huruma na maendeleo ya Kiuchumi.
Kuwahimiza kushiriki utoaji na Hazina ya Mwanamke kwa ajili ya Utendaji na Uwajibikaji wa Utume wa Mwanamke Mkatoliki.
Kuandaa vikao vya Kamati ya WAWATA.
Kuwahimiza Wanawake wa Parokia kushiriki katika maazimio mbali mbali ya Kiparokia na Kijimbo.
Kufanya vikao na Semina kuunganisha wawakilishi wa WAWATA kutoka Jumuiya Ndogo Ndogo.
Kuwahimiza kushiriki mchango wa Kituo cha Malezi ya Vijana Jimboni.
Kuandaa vikao vya wawakilishi na Kamati Tendaji ya WAWATA Kiparokia.
Kushiriki vikao vinavyoandaliwa na WAWATA Jimbo Kuu.
Kuhudhuria vikao vya Baraza la kichungaji / Halmashauri ya Utekelezaji Parokia.

MAJUKUMU YA KAMATI YA VIJANA NA MIITO
Kuhimiza Vijana kujiunga katika vikundi vya vijana. Parokiani, ambavyo ni Mt. Aloyce na VIWAWA.
Kuratibu Semina mbali mbali za kuwasaidia Vijana kuelewa nafasi yao katika Kanisa na hatima ya miito yao.
Kuandaa matamasha, makongamano na mafungo na mengineyo kwa ajili ya Vijana.
Kufanya vikao na Semina kuunganisha wawakilishi wa Vijana na Miito kutoka Jumuiya Ndogo Ndogo.
Kuandaa vikao mbali mbali vya Vijana Parokiani.
Kuhudhuria vikao vya Halmashauri ya Utekelezaji Parokia.

MAJUKUMU YA KAMATI YA FEDHA, UCHUMI NA MIPANGO
Kuweka kumbukumbu zote za mali na fedha za Parokia.
Kusimamia miradi yote ya Parokia (kama ipo)
Kubuni njia mbalimbali zinazotekelezeka za kuinua uchumi wa Parokia.
Kuandaa bajeti ya Parokia na kuwakilisha kwenye Kamati Tendaji ya Parokia.
Kutengeneza makisio ya mapato na matumizi ya Parokia kila mwaka.
Kutengeneza taarifa ya mapato na matumizi kila mwezi na kuiwasilisha kwa Kamati Tendaji.
Kufanya vikao na Semina kuunganisha wawakilishi wa Watunza Hazina  kutoka Jumuiya Ndogo Ndogo.
Kushughulikia maslahi yote ya Parokia kwa Wafanyakazi. (ajira, nidhamu, mishahara, likizo n.k.).
Kudhibiti matumizi ya fedha na mali ya Parokia na  Kuandaa vikao vya Kamati ya Fedha Uchumi na Mipango
Kuhudhuria vikao vya Baraza la Kichungaji / Halmashauri ya Utekelezaji Parokia pamoja na Halmashauri ya Parokia.

MAJUKUMU YA KAMATI YA  WASIOJIWEZA
Kutambua vitengo vinavyohusika na wasiojiweza katika Parokia yetu.
Kutambua vyanzo vya fedha na misaada kwa ajili ya kusaidia wenye shida Parokiani.
Kubuni mbinu za kuanzisha mfuko wa wasiojiweza Parokiani.
Kufanya vikao na Semina kuunganisha wawakilishi wa wasiojiweza kutoka Jumuiya Ndogo Ndogo.
Kuweka mfumo au utaratibu mzuri wa kuhudumia wenye shida.
Kubuni siku moja katika mwaka kwa ajili ya sikukuu ya Wasiojiweza.
Kuandaa Vikao vya Kamati ya wasiojiweza.
Kuandaa na kusimamia maadhimisho ya sikukuu ya wasiojiweza - Siku ya Huruma ya MUNGU – kila mwaka.
Kuhudhuria vikao vya Halmashauri ya Utekelezaji Parokia.

MAJUKUMU YA SHIRIKISHO LA KWAYA
Kuandaa mikutano, semina na mafungo kwa ajili ya Kwaya zote ili kudumisha upendo, haki na amani kati yao.
Kuhimiza Kwaya zote kujituma vilivyo katika kazi ya uenezaji Injili kwa njia ya nyimbo wakati wowote na mahali popote pindi watakiwapo kufanya hivyo.
Kuhimiza Kwaya zote ziwe na Akaunti benki na kushughulikia vilivyo mapato na matumizi yao.
Kuhimiza Kwaya zote kuwa na ratiba ya vikao kwa ajili ya maendeleo na majukumu yao ya kila siku.
Kubuni mbinu mbali mbali za Kiuchumi za kuboresha Kwaya na Shirikisho pia.
Kuhakikisha nyimbo za kwenye Ibada za Misa zinafuata Liturujia.
Kutunza nidhamu pindi wawapo nje ya Parokia kiutume.
Kuandaa Vikao vya Shirikisho la Kwaya.
Kuhudhuria vikao vya Baraza la Kichungaji / Halmashauri ya Utekelezaji Parokia

MAJUKUMU YA KAMATI YA SHIRIKISHO LA VYAMA VYA KITUME PAROKIANI
Kuhimiza kila chama kiwe na Katiba yake na kila mwanachama kupata nakala ili aisome, aielewe na kuitekeleza.
Kuandaa Semina, makongamano au warsha mbali mbali za Shirikisho.
Kuhimiza kila Chama au Shirika linaadhimisha sikukuu ya somo wao kwa Misa Takatifu kila mwaka baada ya maandalizi ya kiroho kama vile semina, mafungo na kupokea Sakramenti ya Kitubio.
Kubuni mbinu mbali mbali za kiuchumi ili kuboresha utendaji wa Vyama na Shirikisho pia.
Kuandaa utaratibu wa vikao vya Shirikisho la Vyama vya Kitume.
Kuhudhuria vikao vya Halmashauri ya / Baraza la Kichungaji



Post a Comment

 
Top