KANISA KATOLIKI LA MT. FRANSISKO KSAVERI
PAROKIA YA OLOSIPA
KALENDA YA SHUGHULI ZA KICHUNGAJI
JANUARI 2015 HADI DESEMBA 2015

JANUARI

01-01-2015: Alhamisi- Mwaka Mpya
  • Umama wa BIKIRA MARIA (I. Hes 6:22-27; II.Gal 4:4-7; III. Lk 2:16-21).
  • Misa moja saa 1:00 asubuhi.

04-01-2015. Dominika ya Tokeo la BWANA. (I. Isa 60:1-6; II. Efe 3:2-3, 5-6; III. Mt 2:1-12)
·         Siku ya kubariki nyumba zote za waamini wa Parokia ya Mt. Fransisko Ksaveri. Waamini walete maji, chumvi, ubani na chaki kwa ajili ya baraka ya nyumba. 
·         Tangazo la kwanza kwa watoto wanaopenda kujiunga na seminari kwa nia ya kuwa mapadre.  Watoto wote wanaopenda kujiunga na seminari wapitie kwa viongozi wa Jumuiya Ndogo ndogo.  Viongozi wafike ofisini mapema kuchukua fomu za kuwapendekeza watoto hao.  Watoto wawe wa darasa la saba.
·         Matoleo ya pili kwa ajili ya Seminari.

08-01-2015. Alhamisi ya kwanza ya mwezi
·         Kuabudu Ekaristi Takatifu kwa kimya kuanzia saa 1: 00 asubuhi mara tu baada ya misa na kuhitimishwa kwa Masifu ya Jioni na Baraka ya Sakramenti Kuu saa 11:00 kamili.

11-01-2015. Dominikaya Ubatizo wa BWANA (I.Isa 55:1-11; II. Yo 5:1-9; III. Mk 1:7-11)
  • Tangazo la pili kwa watoto wanaopenda kujiunga na seminari kwa nia ya kuwa mapadre.  Watoto wote wanaopenda kujiunga na seminari wapitie kwa viongozi wa Jumuiya Ndogo ndogo.  Viongozi wafike ofisini mapema kuchukua fomu za kuwapendekeza watoto hao.  Watoto wawe wa darasa la saba.

18-01-2015. Dominika ya 2 ya Mwaka B. (I. 1 Sam 3:3b-10,19; II. 1 Kor 6:13c-15a. 17-20; III. Yn 1:35-42)
  • Mkutano wa Halmashauri Parokia mara tu baada ya misa ya kwanza.

19-01-2015. Jumatatu
  • Mwanzo wa mafundisho ya Watoto wanaojiandaa kwa Komunyo ya Kwanza na Kipaimara saa 10:00 jioni.

25-01-2015. Dominika ya 3 ya Mwaka B. (I. Yon 3: 1-5, 10; II. 1 Kor 7:29-31; II. Mk 1:14-20)
26-01-2015. Jumatatu
  • Misa na Neno la Kiroho kwa wanakwaya wa Kwaya zote saa 11:00 jioni.

30-01-2015. Ijumaa
  • Kikao cha Kamati Tendaji saa 11:30 jioni kwenye Ofisi ya Parokia.

FEBRUARI

01-02-2015. Dominika ya 4 ya Mwaka B. (I. Kum 18:15-20; II. 1 Kor 7:32-35, III. Mk 1:21-28)
  • Utegemezaji wa Kanisa, ni zamu ya Jumuiya ya Wat. Petro na Paulo Mitume.
  • Sadaka ya pili kwa ajili ya Mfuko wa Askofu Denis Durning.

02-02-2015. Jumatatu, Kumtolea BWANA Hekaluni.  (I. Mal 3:1-4; II. Ebr 2:14-18; III. Lk 2:22-40)
  • Misa itaanza saa 12:30 asubuhi ambapo kutakuwepo na maandamano ya mishumaa kama ilivyobainishwa katika Misale ya Altare Uk. 215.  Waamini wafike na mishumaa na kujitokeza kwa wingi.

03-02-2015. Jumanne. Sikukuu ya Mtakatifu Blasius
  • Kutakuwepo na ibada ya kubariki shingo ambayo itatolewa kwenye misa ya asubuhi saa 12:30 kwa ajili ya kukinga na kuponya magonjwa yote ya koo.  Waamini tunaombwa kujitokeza kwa wingi.

05-02-2015. Alhamisi ya kwanza ya mwezi
·         Kuabudu Ekaristi Takatifu kwa kimya kuanzia saa 1: 00 asubuhi mara tu baada ya misa na kuhitimishwa kwa Masifu ya Jioni na Baraka ya Sakramenti Kuu saa 11:00 kamili.

07-02-2015. Jumamosi
  • Misa ya Mtaa – Mtaa wa Yerusalemu; saa 12:30 asubuhi.

08-02-2015. Dominika ya 5 ya Mwaka B. (I. Ayu 7:1-4; II. 1Kor 9:16-19, 22-23; III. Mk. 1:29-39)

09-02-2015. Jumatatu
  • Misa ya somo katika Jumuiya ya Mt. Josephine Bakita. Saa 11:00 jioni.  (Sikukuu yake haswa ni kila tarehe 8 Februari.

13-02-2015. Ijumaa
  • Mkesha Mtakatifu wa Kuabudu Ekaristi Takatifu pamoja na Neno la Kiroho na Sakramenti ya Upatanisho. Mkesha utaanza saa 3:00 usiku na kuhitimishwa kwa Ibada ya Misa Takatifu saa 12:00 asubuhi.  Waamini tujitokeze kwa wingi.

14-02-2015. Jumamosi
  • Misa katika Jumuiya ya Mt. Augustino saa 12:30 asubuhi.

15-02-2015. Dominika ya 6 ya Mwaka B. (I. Law 13:1-2, 44-46; II. 1Kor 10:31-33, 11:1; III. Mk 1:40-45)
  • Siku ya Kuwekwa Wakfu Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki Arusha.
  • Matoleo ya pili kwa ajili ya Seminari.
  • Misa itakuwa moja ya saa 12.30 asubuhi.
  • Siku ya kutoa sadaka zetu za Shukrani Kijumuiya kwa kumshukuru MUNGU kwa kumaliza Mwezi wa pili salama.
  • Kikao cha Paroko na Wazazi na Walezi wote wa wanafunzi wa Sakramenti ya Ekaristi na Kipaimara. Kikao kitafanyika mara tu baada ya Misa ya pili.  Wazazi na walezi washiriki Ibada ya Mis ya pili.

Maungamo ya kwa kujiandaa na Mfungo Mtakatifu wa Kwaresma

16-02-2015. Jumatatu
  • Maungamo ya Jumla kwa watoto kujiandaa na Mfungo Mtakatifu wa Kwaresma.  Maungamo yataanza saa 10:30.
  • Kikao cha Kamati ya Vijana na Miito.  Kikao kitafanyika saa 11:00 jioni.

17-02-2015. Jumanne
  • Maungamo ya Jumla kwa watu wazima kwa ajili ya kujiandaa kwa Mfungo Mtakatifu wa Kwaresma.  Maungamo yataanza saa 11:00 Wanakwaya wataongoza waamini katika uimbaji.
  • Kumbukumbu ya kifo cha Marehemu Askofu Denis Durning.

18-02-2015. Jumatano ya Majivu (I. Yoe 212-18; II. 2Kor 5:20-6:2; III. Mt 61-6, 16-18)
·         Jumatano ya Majivu, ni siku ya toba ambayo hufanywa kwa kufunga na kujinyima kula nyama.  Ni mwanzo wa kipindi kitakatifu cha Kwaresima.  Misa zitakuwa mbili.  Misa ya kwanza saa 12:30 asubuhi, misa ya pili saa 11:00 jioni. Majivu yatabarikiwa na kuwapaka waamini katika kila misa. Kwaya itawaongoza waamini katika misa ya jioni.
·         Katika kipindi chote cha Kwareisma, kutakuwepo na ibada ya Njia ya Msalaba kila siku za Ijumaa saa 12:00 asubuhi  ikifuatiwa na Ibada ya Misa Takatifu, na Saa 11:00 jioni ikifuatiwa pia na Ibada ya Misa Takatifu.  Na kwa kila Ibada ya Njia ya Msalaba, kutakuwepo na Matoleo maalumu kwa ajili ya Kampeni ya Kwaresima. Waamini tujitahidi sana kushiriki ibada ya Njia ya Msalaba bila kukosa.

21-02-2015. Jumamosi
  • Misa katika Jumuiya ya Mt. Monika saa 12:30 asubuhi.

22-02-2015. Dominika ya 1 ya Kwaresima Mwaka B (I. Mwa 9:8-15; II. 1 Pet 318-22; III. Mk 1:12-15)
  • Utegemezaji wa Kanisa, ni zamu ya Jumuiya ya Moyo Mtakatifu wa YESU.
  • Kugawa bahasha za Majinyimo katika Kipindi cha Kwaresma.  Bahasha hizo zitarudishwa rasmi siku ya Alhamisi Kuu na kupokelewa Paroko.
  • Dominika ya kuwasilisha michango ya Usafi wa Kanisa toka kila Jumuiya shilingi 15,000/=.

23-02-2015. Jumatatu
  • Misa na Neno la Kiroho kwa wanakwaya wa Kwaya zote saa 11:00 jioni.

27-02-2015. Ijumaa
  • Kikao cha Kamati Tendaji saa 11:30 jioni kwenye Ofisi ya Parokia.

28-02-2015. Jumamosi
  • Misa ya Mtaa – Mtaa wa Bethania; saa 12:30 asubuhi.

MARCHI

01-03-2015. Dominikaya 2 ya Kwaresima (I. Mwa 22:51-2, 9a, 10-13, 15-18; II. Rum 8:31b-34; III. Mk 9:-2- 10)
·         Ibada ya uteuzi au kuandikishwa majina kwa Wakatekumuni (Uk 33). Ibada hii itafanyika misa ya kwanza.
  • Matoleo ya pili kwa ajili ya Mfuko wa Afya ya Mapadre.
  • Siku ya kutoa sadaka zetu za Shukrani Kijumuiya kwa kumshukuru MUNGU kwa kumaliza Mwezi wa pili salama.

05-03-2015. Alhamisi ya kwanza ya mwezi
·         Kuabudu Ekaristi Takatifu kwa kimya kuanzia saa 1: 00 asubuhi mara tu baada ya misa na kuhitimishwa kwa Masifu ya Jioni na Baraka ya Sakramenti Kuu saa 11:00 kamili.

07-03-2015. Jumamosi
  • Misa ya Mtaa – Mtaa wa Galilaya; saa 12:30 asubuhi.

8- 03-2015.  Dominika ya 3 ya Kwaresima (I. Kut 20:1-17; II I Kor 1:22-25; III. Yn 2:13-25)
  • Ibada ya Mazinguo na baraka kwa Wakatekumeni (Uk 13 na 18). Pamoja naibada ya Efata (Uk 30). Ibada hizizitafanyika kwenye misa ya kwanza.
  • Matoleo ya pili kwa ajili ya Seminari.
  • Utegemezaji wa Kanisa, ni zamu ya Jumuiya ya Mt. Yosefu Mfanyakazi.

14-03-2015. Jumamosi
  • Misa katika Jumuiya ya Mt. Klara wa Asizi saa 12:30 asubuhi.

15-03-2015.Dominika ya 4 ya Kwaresima Mwaka B. (2Nya 36:14-16, 19-23; II. Efe 2:4-10; III.Yn 3:14-21)
  • Takaso la Kwanza kwa Wakatekumeni. (Uk 41), na ibada ya Kanuni ya imani (Uk 24).  Ibada hiziz itafanyika kwenye misa ya kwanza.
  • Kikao cha Paroko na Wazazi na Walezi wote wa wanafunzi wa Sakramenti ya Ekaristi na Kipaimara. Kikao kitafanyika mara tu baada ya Misa ya pili.  Wazazi na walezi washiriki Ibada ya Mis ya pili.

21-03-2015. Jumamosi
  • Misa katika Jumuiya ya Mt. Yohane Mbatizaji saa 12:30 asubuhi.

22-03-2015.Dominika ya 5 ya Kwaresima Mwaka B. (I. Yer 31:31-34; II. Ebr 5:7-9; III. Yn 12:20-33)
  • Takaso la Pili kwa Wakatekumeni (Uk 46). 

23-03-2015. Jumatatu
  • Ibada ya baraka maalum kwa kina mama wote wajawazito.  Baraka hiyo itatolewa saa 11:00 jioni hapa kanisani.  Kina mama wote wajawazito wafike kwenye ibada hiyo kwa nia ya kuwabariki na kumwomba MUNGU ili waweze kujifungua salama.

27-03-2015. Ijumaa
  • Kikao cha Kamati Tendaji saa 11:30 jioni kwenye Ofisi ya Parokia.

28-03-2015. Jumamosi
  • Misa ya Mtaa – Mtaa wa Nazareti; saa 12:30 asubuhi.
  • Mafundisho kwa Wazazi na Wasimamizi wa watoto wa ubatizo, saa 11:00 jioni kwenye Kanisa dogo.  Wazazi / Walezi wote wawili wahakikishe wanahudhuria mafundisho hayo pamoja na wasimamizi.

29-03-2015. Dominika ya Matawi. (I. Isa 50:4-7; II Flp 2:6-11; III. Mk 14:1-15:47)
  • Mkutano wa Halmashauri Parokia mara tu baada ya misa ya kwanza.
  • Dominika ya Matawi ya Mateso ya BWANA.  Siku ambayo Kanisa linaingia kwenye mafumbo ya Kifo, Kuzikwa na Ufufuko wa BWANA wake.
  • Siku hiyo kutakuwepo na misa 1. Kutakuwepo na maandamano ya shangwe kukumbuka kuingia kwa BWANA Yerusalemu.  Waamini watakusanyika kwenye eneo la bombani, ambapo matawi yatabarikiwa na kisha maandamano yataanzia hapo kuelekea Kanisani tayari kwa ibada ya Misa.    Kila mwamini alete tawi lake. 
  • Dominika hii ni sikukuu ya vijana kote ulimwenguni.  Kutakuwepo naMatoleo ya pili kwa ajili ya utume wa Vijana jimboni.
  • Vijana wote wataungana na vijana wenzao wa Jimbo kwenda kwenye Hija huko Kanani, Kisongo wakiungana na Baba Askofu Mkuu.  Vijana wote wanaombwa kushiriki.
  • Takaso la Tatu kwa Wakatekumeni (Uk 50).  Ibada hii itafanyika kwenye misa ya kwanza.
  • Siku ya kugawa bahasha kwa ajili ya Matoleo Maalumu ya Pasaka, kukumbuka sikukuu ya Ukombozi wetu.
  • Utegemezaji wa Kanisa, ni zamu ya Jumuiya ya Mt. Josephina Bakita.
  • Dominika ya kuwasilisha michango ya Usafi wa Kanisa toka kila Jumuiya shilingi 15,000/=.

30-03-2015. Jumatatu
  • Misa na Neno la Kiroho kwa wanakwaya wa Kwaya zote saa 11:00 jioni.

Maungamo kwa ajili ya kujiandaa na sikukuu ya Pasaka

31-03-2015. Jumnne
  • Maungamo ya Jumla kwa watoto, yataanza saa 10:30 jioni, Kanisani.

APRILI

01-04-2015. Jumatano
  • Maungamo ya Jumla kwa watu wazima wote, yakifuatiwa na Ibada ya Misa Takatifu.  Maungamo yataanza saa 11:00 Jioni.  Kila mwamini atatakiwa kufika na mshumaa.

SIKU TATU KUU ZA PASAKA

02-04-2015.  ALHAMISI KUU JIONI: KARAMU YA BWANA
  • Misa ya Karamu ya BWANA itaanza saa 11 :00 jioni.
  • Watakaooshwa miguu ni waamini wanaume 12 watakaochaguliwa na Kamati ya Liturujia.
  • Siku hiyo ni siku ya kuleta kile tulichojinyima wakati wa kipindi chote cha Kwaresma.
  • Baada ya Misa ya karamu ya BWANA, kutafuata kuabudu tukianzia Mtaa wa Betlehemu kuanzia saa 1:00 hadi saa 2:00; Mtaa wa Yerusalemu kuanzia saa 2.00 hadi saa 3:00; Mtaa wa Nazareti kuanzia saa 3:00 hadi saa 4:00; Mtaa wa Bethania, kuanzia saa 4:00 hadi saa 5:00.  Mtaa wa Galilaya kuanzia saa 5:00 hadi saa 6:00.  Viongozi wa Mitaa wakishirikiana na viongozi wa Jumuiya Ndogo ndogo wawahamasishe waamini kujitokeza kwa wingi na kupanga utaratibu wa kuabudu pamoja na nyimbo zitakazotumika.

03-04-2015. IJUMAA KUU YA MATESO YA BWANA
  • Ibada ya Mateso ya BWANA itaadhimishwa saa 9:00 kamili alasiri, ikitanguliwa na Ibada  ya Njia ya Msalaba.
  • Matoleo ya siku hiyo ni kwa ajili ya Nchi Takatifu.
  • Mwanzo wa Novena ya “Huruma ya MUNGU”.  Novena hiyo itasaliwa baada ya Ibada ya Njia ya Msalaba.
  • Siku hii ni ya kutokula nyama kwa waamini. Ni amri ya Kanisa.

04-04-2015. JUMAMOSI KUU
·         Adhimisho la Mkesha wa Pasaka, litaanza saa 2:00 kamili za usiku.
·         Jumuiya ya Mt. Teresia wa Mtoto YESU, wataandaa kuni na kuwasha moto wa Pasaka.  Kadiri inavyowezekana moto mkubwa uandaliwe nje ya kanisa hivi kwamba miali yake itawanye kweli giza na iangaze usiku.
·         Watangazaji wa Masomo Matakatifu waandae masomo yote.  Kwani katika Kesha la Paska masomo yote yatasomwa kama Liturujia inavyoelekeza.
·         Kwenye Kesha hilo, Wakatekumeni watabatizwa na kupata kipaimara.  Kutakuwepo na tendo rasmi la kuwakabidhi Wakatekumeni hao kwa Wenyeviti wao wa Jumuiya ili kuhakikisha malezi endelezi ya Kiroho wanapatiwa na wanajumuiya husika.
·         Baraka ya Vyakula vya Pasaka itatolewa.  Waamini waje na sehemu ndogo ya vyakula vitakavyoliwa Pasaka ili vibarikiwe.  Vitu kama unga, mchele, mayai, mkate, mafuta n.k, ili waamini wavitumiapo wapate kutakaswa pia mwilini.
·         Waamini watakaohudhuria Mkesha wa Pasaka, wanatakiwa kufika wakiwa na mishumaa yao.
·         Novena ya “Huruma ya MUNGU” itasaliwa kabla Saa 2:00 asubuhi.
·         Ndoa za jumla kwa waamini waliojiandikisha na kupata mafundisho zitaadhimishwa.
  • Siku ya kutoa sadaka zetu za Shukrani Kijumuiya kwa kumshukuru MUNGU kwa kumaliza Mwezi wa pili salama.

05-04-2015. Dominika ya Pasaka.UFUFUKO WA BWANA (I. Mdo. 10:34; 37-43; II. Kol 3:1-4; III. Yn 20:1-9)
·         Misa zitakuwa mbili. Misa ya kwanza itaanza saa 12:30 asubuhi.  Misa ya pili saa 3:00 asubuhi. Misa ya watoto haitakuwepo ili kuruhusu watoto kusherehekea sikukuu na wawazi / walezi wao.
·         Baraka ya vyakula vya Pasaka itatolewa katika Ibada ya Misa ya Kwanza.
·         Novena ya “Huruma ya MUNGU” itasaliwa kabla ya misa kumalizika.

06-04-2015.  Jumatatu ya Pasaka. (I.Mdo. 2:14, 22-33; II. Mt 28:8-15)
·      Misa itakuwa moja na itaanza saa moja asubuhi. Novena ya “Huruma ya MUNGU” itasaliwakabla ya Ibada ya misa.
·      Wanakwa wote wa kwaya zote za Jimbo, watakuwa na misa ya pamoja na Baba Askofu Mkuu.  Ni sikukuu ya Wanakwaya Kijimbo.
·      Ubatizo wa Watoto wachanga.

07-04-2015.                                                 Jumanne katika Oktava ya Pasaka. (I. Mdo. 2:14; 36-41; II. Yn 20:11-18)
Novena ya “Huruma ya MUNGU”itasaliwa  kabla ya Ibada ya misa ya  saa 12:30 asubuhi.

08-04-2015. Jumatano katika Oktava ya Pasaka. (I. Mdo. 3:1-10; II. Lk 24:13-35)
Novena ya “Huruma ya MUNGU” itasaliwa kabla ya Ibada ya misa ya saa 12:30 asubuhi.

09-04-2015. Alhamisi katika Oktava ya Pasaka. (I. Mdo. 3:11-26; II. Lk 24:35-48)
Novena ya “Huruma ya MUNGU” itasaliwa kabla ya Ibada ya misa ya saa 12:30 asubuhi.

10-04-2015. Ijumaa  katika Oktava ya Pasaka. (I. Mdo. 4:1-12; II. Yn 21:1-14) 
·      Novena ya “Huruma ya MUNGU” itasaliwa kabla ya Ibada ya misa ya saa12:30 asubuhi.
11-04-2015.Jumamosi katika Oktava ya Pasaka. (I. Mdo. 4:13-21; II. Mk 16:9-15)
·      Novena ya “Huruma ya MUNGU”itasaliwa kabla ya Ibada ya Rozari Takatifu saa 10:30 jioni.
  • Misa katika Jumuiya ya Mt. Fransisko wa Asizi saa 12:30 asubuhi

12-04-2015. Dominika ya 2 ya Pasaka Mwaka B. (I. Mdo. 4:32-35; II. Yo 3:1-6; III. Yn 20:19-31)
  • Sikukuu ya Huruma ya MUNGU.
  • Ni siku ambapo waamini wanaalikwa kutoa Matoleo maalumu kwa ajili ya  wasiojiweza, wafungwa na wagonjwa.  Vitu kama fedha, sabuni, dawa za meno, miswaki, mafuta ya kujipaka, matunda, nguo, nafaka nk. vinaweza kutolewa.  Parokia itatembelea Kituo cha Watoto yatima Kisongo pamoja na Magereza ili kuwapelekea vitu hivyo.
  • Utegemezaji wa Kanisa, ni zamu ya Jumuiya ya Mt. Yohani Paulo II.

18-04-2015. Jumamosi
  • Misa katika Jumuiya ya Mt. Baltazari saa 12:30 asubuhi.

19-04-2015. Dominika ya 3 ya Pasaka Mwaka B. (I. Mdo. 3:13-15, 17-19a; II. 1Yo 2:1-5a; III. Lk. 24-35-48)
  • Uhamasisho wa Sikukuu ya Wafanyakazi ili kila mwamini alete kifaa chake cha kufanyia kazi kwa ajili ya kubarikiwa.
  • Matoleo ya pili kwa ajili ya Seminari.
  • Kikao cha Paroko na Wazazi na Walezi wote wa wanafunzi wa Sakramenti ya Ekaristi na Kipaimara. Kikao kitafanyika mara tu baada ya Misa ya pili.  Wazazi na walezi washiriki Ibada ya Mis ya pili.

24-04-2015. Ijumaa
  • Kikao cha Kamati Tendaji saa 11:30 jioni kwenye Ofisi ya Parokia.

25-04-2015. Jumamosi
  • Misa ya Mtaa – Mtaa wa Bethlehemu; saa 12:30 asubuhi.

26-04-2015. Dominika ya 4 ya Pasaka. (I. Mdo. 4:8-12; II. 1Yo 3:1-2; III. Yn 10:11-18)
  • Kumbukumbu ya Kutabarukiwa Kanisa la Parokia nan i siku ambapo Parokia ilipoanzishwa rasmi.
  • Matoleo ya pili kwa ajili ya Miito.
  • Ibada ya kuwakaribisha na kuwapokea rasmi wageni wote waliohamia na kujiunga na Parokia yetu kuanzia mwezi wa kwanza 2015.
  • Dominika ya kuwasilisha michango ya Usafi wa Kanisa toka kila Jumuiya shilingi 15,000/=.

27-04-2015. Jumatatu
  • Misa na Neno la Kiroho kwa wanakwaya wa Kwaya zote saa 11:00 jioni.

29-04-2015. Ijumaa
  • Misa ya somo katika Jumuiya ya Mt. Yosefu Mfanyakazi. Saa 11:00 jioni. 

MEI

01-05-2015.  Ijumaa; Sikukuu ya Wafanyakazi
Misa itakuwa moja saa 1.00 asubuhi. Kutakuwepo na baraka ya kubariki vyombo vya kazi.  Waamini wote wanatakiwa kuja na vyombo vyao vya kufanyia kazi kwa baraka. Katika wiki hiyo baraka kwa ofisi za waamini pamoja na sehemu zao za kazi pia zitatolewa. Kwa wale wanaohitaji, Wanaombwa kuonana na padre kabla ili kuleta ufanisi.

02-05-2015. Jumamosi
  • Misa ya Mtaa – Mtaa wa Yerusalemu; saa 12:30 asubuhi.

03-05-2015.  Dominika ya 5 ya Pasaka. (I. Mdo. 9:26-31; II. 1Yo 3:18-24; Yn 15:1-8)
  • Ziara ya Majifunzo kwa wajumbe wa Kamati Tendaji na Kamati ya Fedha, Uchumi na Mipango kutembelea Parokia ya Kijenge.  Watashiriki Misa ya Kwanza Kijenge.
  • Siku ya kutoa sadaka zetu za Shukrani Kijumuiya kwa kumshukuru MUNGU kwa kumaliza Mwezi wa pili salama.

07-05-2015. Alhamisi ya kwanza ya mwezi
·         Kuabudu Ekaristi Takatifu kwa kimya kuanzia saa 1: 00 asubuhi mara tu baada ya misa na kuhitimishwa kwa Masifu ya Jioni na Baraka ya Sakramenti Kuu saa 11:00 kamili.

09-05-2015. Jumamosi
  • Misa katika Jumuiya ya Mt. Antoni wa Padua saa 12:30 asubuhi.

10-05-2015.  Dominika ya 6 ya Pasaka. (Mdo. 10:25-26, 34-35, 44-48; II. 1Yo 4:7-10; III. Yn 15:9-17)
  • Matoleo ya Pili kwa ajili ya Seminari yetu ya Jimbo Kuu la Arusha.
  • Utegemezaji wa Kanisa, ni zamu ya Jumuiya ya Mt. Sesilia.

15-05-2015. Ijumaa
  • Mkesha Mtakatifu wa Kuabudu Ekaristi Takatifu pamoja na Neno la Kiroho na Sakramenti ya Upatanisho. Mkesha utaanza saa 3:00 usiku na kuhitimishwa kwa Ibada ya Misa Takatifu saa 12:00 asubuhi.  Waamini tujitokeze kwa wingi.

17-05-2015. Kupaa kwa BWANA (I. Mdo. 1:1-11; II. Efe 1:17-23; III. Mk 16:15-20)
  • Kikao cha Paroko na Wazazi na Walezi wote wa wanafunzi wa Sakramenti ya Ekaristi na Kipaimara. Kikao kitafanyika mara tu baada ya Misa ya pili.  Wazazi na walezi washiriki Ibada ya Mis ya pili.

23-05-2015. Jumamosi
  • Misa ya kesha la Sikukuu ya Pentekoste.  Misa itaadhimishwa saa 11:00 jioni.
  • Misa katika Jumuiya ya Mt. Inyasi wa Loyola saa 12:30 asubuhi.

24-05-2015. Sikukuu ya Pentekoste. (I. Mdo. 2:1-11; II. 1 Kor 12:3-7, 12-13; III. Yn 20:19-23)
  • Matoleo ya kwanza siku hiyo ni kwaajili ya Baraza la Walei – Jimbo.

25-05-2915. Jumatatu
  • Misa na Neno la Kiroho kwa wanakwaya wa Kwaya zote saa 11:00 jioni.

29-05-2015. Ijumaa
  • Kikao cha Kamati Tendaji saa 11:30 jioni kwenye Ofisi ya Parokia.

30-05-2015. Jumamosi
  • Misa ya Mtaa – Mtaa wa Bethania; saa 12:30 asubuhi.

31-05-2015. Sikukuu ya Utatu Mtakatifu. (I. Kum 4:32-34; II. Rum 8:14-17; III. Mt. 28:16-20)
  • Matoleo ya Pili kwa ajili ya Chuo Kikuu cha Afrika Mashariki (Catholic University of East Africa).
  • Utegemezaji wa Kanisa, ni zamu ya Jumuiya ya Mt. Inyasi wa Loyola.
  • Dominika ya kuwasilisha michango ya Usafi wa Kanisa toka kila Jumuiya shilingi 15,000/=.

JUNI

04-06-2015. Alhamisi ya kwanza ya mwezi
·         Kuabudu Ekaristi Takatifu kwa kimya kuanzia saa 1: 00 asubuhi mara tu baada ya misa na kuhitimishwa kwa Masifu ya Jioni na Baraka ya Sakramenti Kuu saa 11:00 kamili.

06-06-2015. Jumamosi
  • Misa ya Mtaa – Mtaa wa Galilaya; saa 12:30 asubuhi.

07-06-2015. MWILI na DAMU ya KRISTO. (I. Kut 24:3-8; II. Ebr 9:11-15; III. Mk 14:12-16, 22-26)
  • Matoleo ya pili kwa ajili ya Mt. Patro (Peter’s Pence).
  • Siku hiyo Misa itakuwa 1. Itakayoanza saa 1 : 00 asubuhi.    Mara tu baada ya misa maandamano ya Ekaristi Takatifu sana yataanza.  Maandamano hayo ya Bikira MARIA yataanza hapa Kanisani na kuishia Parokia ya Mt. Monika kwa kupitia Ofisi ya Kijiji, Raskazoni, Getini na kuelekea Parokiani Mt. Monika.
  • Siku ya kutoa sadaka zetu za Shukrani Kijumuiya kwa kumshukuru MUNGU kwa kumaliza Mwezi wa pili salama.

N.B. Baada ya Dominika hii hakutakuwepo na Sadaka ya Shukrani kwa kila mwezi ili kuruhusu waamini kujiandaa na Sikukuu ya Shukrani / Mazao mwezi wa 12 wakati wa Sikukuu ya Somo wa Parokia 6-12-2015

12-06-2015. Ijumaa
  • Adhimisho la Misa katika Jumuiya ya Moyo Mt. wa YESU, Somo wa Jumuiya.  Adhimisho litaanza saa 11:00.

13-06-2015. Jumamosi
  • Sikukuu ya Somo wa Jumuiya ya Mt. Antoni wa Padua.  Misa saa 11:00 Jioni.

14-06-2015. Dominika ya 11 ya Mwaka B. ( I. Eze 17:22-24; II. 2Kor 5:6-10; II. Mk 4:26-34)
  • Matoleo ya pili kwa ajili ya Seminari.
  • Utegemezaji wa Kanisa, ni zamu ya Jumuiya ya Mt. Benedicto.
  • Kikao cha Paroko na Wazazi na Walezi wote wa wanafunzi wa Sakramenti ya Ekaristi na Kipaimara. Kikao kitafanyika mara tu baada ya Misa ya pili.  Wazazi na walezi washiriki Ibada ya Mis ya pili.

15-06-2015. Jumatatu
  • Ibada ya baraka maalum kwa kina mama wote wajawazito.  Baraka hiyo itatolewa saa 11:00 jioni hapa kanisani.  Kina mama wote wajawazito wafike kwenye ibada hiyo kwa nia ya kuwabariki na kumwomba MUNGU ili waweze kujifungua salama.

20-06-2015. Jumamosi
  • Misa katika Jumuiya ya Wat. Malaika Walinzi saa 12:30 asubuhi.

21-06-2015. Dominika ya 12 ya Mwaka B. ( I. Ayu 38:1,8-11; II. 2Kor 5:14-17; II. Mk 4:35-41)

•23-06-2015. Jumanne
  • Misa ya kesha la Sikukuu ya Kuzaliwa Mt. Yohani Mbatizaji.  Misa itaadhimishwa saa 11:00 jioni.

24-06-2015. Jumatano, Kuzaliwa Mt. Yohani Mbatizaji (I. Isa 49:1-6; II Mdo. 13:16, 22-26; III. Lk 1:57-66, 80)
  • Misa itaadhimishwa kanisani saa 12:30 asubuhi.
  • Sikukuu ya Somo wa Jumuiya ya Mt. Yohani Mbatizaji.  Misa saa 11:00 Jioni.

26-06-2015. Ijumaa
  • Kikao cha Kamati Tendaji saa 11:30 jioni kwenye Ofisi ya Parokia.

27-06-2015. Jumamosi
  • Misa ya Mtaa – Mtaa wa Nazareti; saa 12:30 asubuhi.

28-06-2015. Dominika ya 13 ya Mwaka B. (I. Hek 1:13-15; 2:23-24; II. 2Kor 8:7,9,13-15; III. Mk 5:21-43)
  • Mkutano wa Halmashauri Parokia mara tu baada ya misa ya kwanza.
  • Dominika ya kuwasilisha michango ya Usafi wa Kanisa toka kila Jumuiya shilingi 15,000/=.
  • Utegemezaji wa Kanisa, ni zamu ya Jumuiya ya Mt. Teresia wa Mtoto YESU.

29-06-2015. Jumatatu
  • Sikukuu ya Somo wa Jumuiya ya Wat. Petro na Paulo Mitume.  Misa saa 11:00 Jioni.

30-06-2015. Jumanne
  • Misa na Neno la Kiroho kwa wanakwaya wa Kwaya zote saa 11:00 jioni.

JULAI

02-07-2015. Alhamisi ya kwanza ya mwezi.
·         Kuabudu Ekaristi Takatifu kwa kimya kuanzia saa 1: 00 asubuhi mara tu baada ya misa na kuhitimishwa kwa Masifu ya Jioni na Baraka ya Sakramenti Kuu saa 11:00 kamili.
  • Kumbukumbu ya kifo cha Padre Simon Sirikwa. Misa ya saa 12:30 ni kwa ajili ya kumwombea Pd. Simon Sirikwa na mapadre wote wa Jimbo.

04-07-2015. Jumamosi
  • Misa ya Mtaa – Mtaa wa Bethlehemu; saa 12:30 asubuhi.

05-07-2015. Dominika ya 14 ya Mwaka B. (I. Eze 2:2-5; II. 2Kor 12:7-10; III. Mk 6:1-6)

09-07-2015. Alhamisi
  • Sikukuu ya Somo wa Jumuiya ya Mt. Veronika.  Misa saa 11:00 Jioni.

11-07-2015. Jumamosi
  • Sikukuu ya Somo wa Jumuiya ya Mt. Benedicto.  Misa saa 12:30 asubuhi.

12-07-2015. Dominika ya 15 ya Mwaka B. (I. Amo 7:12-15; II. Efe 1:3-14; III. Mk 6:7-13)
  • Matoleo ya pili Kwa ajili ya Seminari yetu ya Jimbo Kuu la Arusha.
  • Utegemezaji wa Kanisa, ni zamu ya Jumuiya ya Wat. Malaika wakuu.

15-07-2015. Jumatano
  • Mafundisho kwa Wazazi na Wasimamizi wa watoto wa ubatizo, saa 11:00 jioni kwenye Kanisa dogo.  Wazazi / Walezi wote wawili wahakikishe wanahudhuria mafundisho hayo pamoja na wasimamizi.

18-07-2015. Jumamosi
  • Ubatizo wa watoto wachanga saa 4:00 asubuhi.
  • Misa katika Jumuiya ya Wat. Yohakimu na Ana saa 12:30 asubuhi.

19-07-2015. Dominika ya 16 ya Mwaka B. (I. Yer23:1-6; II. Efe 2:13-18; III. Mk 6:30-34)
  • Kikao cha Paroko na Wazazi na Walezi wote wa wanafunzi wa Sakramenti ya Ekaristi na Kipaimara. Kikao kitafanyika mara tu baada ya Misa ya pili.  Wazazi na walezi washiriki Ibada ya Mis ya pili.

25-07-2015. Jumamosi
  • Misa ya Mtaa – Mtaa wa Yerusalemu; saa 12:30 asubuhi.
  • Mtihani wa Kwanza kwa wanafunzi wa Komunyo ya Kwanza saa 3:00 asubuhi.

26-07-2015. Dominika ya 17 ya Mwaka B. (I. 2Fal 4:42-44; II. Efe 4:1-6; III. Yn 6:1-15)
  • Utegemezaji wa Kanisa, ni zamu ya Jumuiya ya Mt. Yuda Tadei.
  • Dominika ya kuwasilisha michango ya Usafi wa Kanisa toka kila Jumuiya shilingi 15,000/=.

27-07-2015. Jumatatu
  • Sikukuu ya Somo wa Jumuiya ya Wat. Yohakimu na Anna.  Misa saa 11:00 Jioni.

28-07-2015. Jumanne
  • Misa na Neno la Kiroho kwa wanakwaya wa Kwaya zote saa 11:00 jioni.

29-07-2015. Jumatano
  • Kikao cha Kamati Tendaji saa 11:30 jioni kwenye Ofisi ya Parokia.

31-07-2015. Ijumaa
  • Sikukuu ya Somo wa Jumuiya ya Mt. Inyasi wa Loyola.  Misa saa 11:00 Jioni.

AGOSTI

01-08-2015. Jumamosi
  • Misa ya Mtaa – Mtaa wa Bethania; saa 12:30 asubuhi.
  • Mtihani wa Kwanza kwa wanafunzi wa Kipaimara saa 3:00 asubuhi.

02-08-2015.Dominika ya 18 ya Mwaka B. (I. Kut 16:2-4, 12-15; II. Efe 4:17,2024; III. Yn 6:24-35)
  • Matoleo ya pili kwa ajili ya Upashanaji Habari yaani Mawasiliano.

06-08-2015. Alhamisi ya kwanza ya mwezi
  • Kuabudu Ekaristi Takatifu kwa kimya kuanzia saa 1: 00 asubuhi mara tu baada ya misa na kuhitimishwa kwa Masifu ya Jioni na Baraka ya Sakramenti Kuu saa 11:00 kamili.

08-08-2015. Jumamosi
  • Misa katika Jumuiya ya Mt. Yuda Tadei saa 12:30 asubuhi.

09-08-2015. Dominika ya 19 (I. 1 Fal. 19:4-8; II Efe. 4:30-5:2, III. Lk. Yn 6:41-51)
  • Matoleo ya Pili kwajili ya Seminari.
  • Utegemezaji wa Kanisa, ni zamu ya Jumuiya ya Wat. Yohakimu na Anna.

15-08-2015. Jumamosi
  • Misa ya kesha ya Kupalizwa Bikira Maria Mbinguni.  Misa itaadhimishwa saa 11:00 jioni.
  • Misa katika Jumuiya ya Mt. Benedicto saa 12:30 asubuhi.

16-08-2015. Kupalizwa  Mbinguni BIKIRA MARIA (I. Ufu 11:19, 12:1-6, 10; II 1Kor 15:20-26, III. Lk 1:39-56)
  • Kikao cha Paroko na Wazazi na Walezi wote wa wanafunzi wa Sakramenti ya Ekaristi na Kipaimara. Kikao kitafanyika mara tu baada ya Misa ya pili.  Wazazi na walezi washiriki Ibada ya Mis ya pili.

21-08-2015. Ijumaa
  • Mkesha Mtakatifu wa Kuabudu Ekaristi Takatifu pamoja na Neno la Kiroho na Sakramenti ya Upatanisho. Mkesha utaanza saa 3:00 usiku na kuhitimishwa kwa Ibada ya Misa Takatifu saa 12:00 asubuhi.  Waamini tujitokeze kwa wingi.

22-08-2015. Jumamosi
  • Misa katika Jumuiya ya Wat. Petro na Paulo Mitume saa 12:30 asubuhi.

23-08-2015. Dominika ya 21 ya Mwaka B. (I. Yos 24:1-2a, 15-18b; II. Efe 5:21-32; III. Yn 6:60-69)

24-08-2015. Jumatatu
  • Ungamo la kwanza kwa watoto wanaojiandaa kupokea Komunyo ya Kwanza.  Maungamo yataanza saa 9.00 alasiri.

26-08-2015. Jumatano
  • Kikao cha Kamati Tendaji saa 11:30 jioni kwenye Ofisi ya Parokia.

27-08-2015. Alhamisi
  • Sikukuu ya Somo wa Jumuiya ya Mt. Monika.  Misa saa 11:00 Jioni.

28-08-2015. Ijumaa
  • Sikukuu ya Somo wa Jumuiya ya Mt. Augustino.  Misa saa 11:00 Jioni.

29-08-2015. Jumamosi
  • Misa ya Mtaa – Mtaa wa Galilaya; saa 12:30 asubuhi.
  • Semina Elekezi kwa wajumbe watakaotembelea Jumuiya kwa nia ya kuhuisha Jumuiya, saa 3.30 asubuhi.

30-08-2015. Dominika ya 22 ya Mwaka B. (I. Kum 4:1-2, 6-8; II. Yak 1:17-18, 21-22, 27; III. Mk 7:1-8, 14-15)
·         Matoleo ya Pili kwa ajili ya Karitasi – Msamaria Mwema.
  • Utegemezaji wa Kanisa, ni zamu ya Jumuiya ya Wat. Malaika Walinzi.
  • Ibada ya kuwatuma Wajumbe watakaotembelea Jumuiya kwa nia ya Kuhuisha Jumuiya.
  • Dominika ya kuwasilisha michango ya Usafi wa Kanisa toka kila Jumuiya shilingi 15,000/=.

31-08-2015. Jumatatu
  • Misa na Neno la Kiroho kwa wanakwaya wa Kwaya zote saa 11:00 jioni.

SEPTEMBA

03-09-2015. Alhamisi ya kwanza ya mwezi
  • Kuabudu Ekaristi Takatifu kwa kimya kuanzia saa 1: 00 asubuhi mara tu baada ya misa na kuhitimishwa kwa Masifu ya Jioni na Baraka ya Sakramenti Kuu saa 11:00 kamili.

05-09-2015. Jumamosi
  • Misa ya Mtaa – Mtaa wa Nazareti; saa 12:30 asubuhi.

06-09-2015. Dominika ya 23 ya Mwaka B.(I. Isa 35:4-7a; II. Yak 2:1-5; III. Mk 7:31-37)
  • Utegemezaji wa Kanisa, ni zamu ya Jumuiya ya Mt. Antoni wa Padua.

12-09-2015. Jumamosi
  • Misa katika Jumuiya ya Moyo Mtakatifu wa YESU saa 12:30 asubuhi.

13-09-2015. Dominika ya 24 ya Mwaka B. (I. Isa 50:5-9; II. Yak 2:14-18; III Mt 8:27-35)
  • Matoleo ya pili kwa ajili ya Seminari yetu ya Jimbo Kuu la Arusha.
  • Kikao cha Paroko na Wazazi na Walezi wote wa wanafunzi wa Sakramenti ya Ekaristi na Kipaimara. Kikao kitafanyika mara tu baada ya Misa ya pili.  Wazazi na walezi washiriki Ibada ya Mis ya pili.

18-09-2015. Ijumaa
  • Mwanzo wa Novena ya Kuhuisha Jumuiya hadi tarehe 26-09-2015.

19-09-2015. Jumamosi
  • Misa katika Jumuiya ya Mt. Yosefu Mfanyakazi saa 12:30 asubuhi.

20-09-2015. Dominika ya 25 ya Mwaka B. (1. Hek 2:12, 17-20; II.Yak 3:16-4:3; Mk 9:30-37)
·         Matoleo ya Pili kwa jili ya Uinjilishaji.
  • Ziara ya Majifunzo kwa wajumbe wa Kamati Tendaji na Kamati ya Fedha, Uchumi na Mipango kutembelea Parokia ya Njiro.  Watashiriki Misa ya Kwanza Njiro.

21-09-2015. Jumatatu
  • Ibada ya baraka maalum kwa kina mama wote wajawazito.  Baraka hiyo itatolewa saa 11:00 jioni hapa kanisani.  Kina mama wote wajawazito wafike kwenye ibada hiyo kwa nia ya kuwabariki na kumwomba MUNGU ili waweze kujifungua salama.

25-09-2015. Ijumaa
  • Kikao cha Kamati Tendaji saa 11:30 jioni kwenye Ofisi ya Parokia.

26-09-2015. Jumamosi
  • Misa ya Mtaa – Mtaa wa Bethlehemu; saa 12:30 asubuhi.
  • Mtihani wa Mwisho kwa wanafunzi wa Komunyo ya Kwanza.
  • Kikao cha Halamshauri Parokia kwa ajili ya kufanya tathimini ya ziara ya kuhuisha Jumuiya saa 3:00 asubuhi.

27-09-2015. Dominika ya 26 ya Mwaka B. (I. Hes 11:25-29; II. 1Yak 5:1-6; III. Mk 9:38-43,45,47-48)
  • Kilele cha mwezi wa Kuhuisha Jumuiya ndogo ndogo.
  • Misa ni moja saa 3:00.
  • Waamini watakuja kwa maandamano kimtaa na kupokelewa na Paroko.
  • Matoleo ya Pili kwa jili ya Mawasiliano.
  • Utegemezaji wa Kanisa, ni zamu ya Jumuiya ya Mt. Baltazari.
  • Dominika ya kuwasilisha michango ya Usafi wa Kanisa toka kila Jumuiya shilingi 15,000/=.

28-09-2015. Jumatatu
  • Misa na Neno la Kiroho kwa wanakwaya wa Kwaya zote saa 11:00 jioni.

29-09-2015. Jumanne
  • Sikukuu ya Somo wa Jumuiya ya Wat. Malaika Wakuu.  Misa saa 11:00 Jioni.

30-09-2015. Jumatano
  • Sikukuu ya Somo wa Jumuiya ya Mt. Teresia wa Mtoto YESU.  Misa saa 11:00 Jioni.

OKTOBA

Mwezi huu ni mwezi wa Rozari Takatifu.  Kwa muda wa mwezi wote huu wa kumi, sala ya Rozari itakuwa ikisaliwa hapa kanisani kila siku baada ya misa ya asubuhi.  Katika mwezi huu wa Rozari, kwa namna ya pekee Mama Kanisa anatualika kuziombea familia zetu, amani, na kumwombea Baba Mtakatifu.  Tunaweza kufanya hivyo kwa kuomba misa kwa nia hizo.  Watu binafsi, Familia, Jumuiya ndogo ndogo, tunahimizwa sana kusali Rozari.  “Familia inayosali pamoja, hukaa pamoja.” Jumuiya zipange utaratibu wa kusali Rozari kila siku kwa muda wa mwezi mzima.

01-10-2015. Alhamisi ya kwanza ya mwezi
  • Kuabudu Ekaristi Takatifu kwa kimya kuanzia saa 1: 00 asubuhi mara tu baada ya misa na kuhitimishwa kwa Masifu ya Jioni na Baraka ya Sakramenti Kuu saa 11:00 kamili.

02-10-2015. Ijumaa
  • Sikukuu ya Somo wa Jumuiya ya Watakatifu Malaika Walinzi.  Misa saa 11:00 Jioni.
  • Mwanzo wa Novena kwa ajili ya Watoto wanaojiandaa kupokea Komunyo ya Kwanza.  Novena itakuwa ikisaliwa kwenye familia za watoto watakaopata Komunyo ya kwanza.

03-10-2015. Jumamosi
  • Misa ya Mtaa – Mtaa wa Yerusalemu; saa 12:30 asubuhi.
  • Ungamo la pili kwa watoto wanaojiandaa kupokea Komunyo ya Kwanza.
  • Mtihani wa Mwisho wa Watoto wa Kipaimara saa 3:00 asubuhi.

04-10-2015. Dominika ya 27 ya Mwaka B. (I. Mwa 2:18-24; II. Ebr 2:9-11; III. Mk 10:2-16)
  • Matoleo ya pili kwa ajili ya AMESEA.
  • Ibada maalumu ya kurudia ahadi za ubatizo kwa Watoto wanaojiandaa kupokea Komunyo ya Kwanza.  Ibada hii itafanyika kwenye misa ya Pili inayoanza saa  3:30 asubuhi.  Wazazi na walezi wawalete watoto wao pamoja na wao wenyewe kushiriki ibada hiyo.

07-10-2015. Alhamisi
  • Ungamo la mwisho kabla ya watoto kupokea Komunyo ya Kwanza pamoja na Wazazi, ndugu jamaa, marafiki na Walezi wao.  Maungamo yataanza saa 9:00 alasiri.

09-10-2015. Ijumaa
  • Ibada ya Misa Takatifu ya kuwaombea Watoto wa Komunyo ya Kwanza na kubariki mavazi yao.  Wazazi, walezi, ndugu na jamaa wote wa watoto wa Komunyo ya Kwanza na wale wote wenye mapenzi mema, wanahimizwa kushiriki Ibada ya Misa hiyo.  Misa itaanza saa 11:00 jioni.

10-10-2015. Jumamosi
  • Misa katika Jumuiya ya Mt. Yohani Paulo II saa 12:30 asubuh.i

11-10-2015. Dominika ya 28 ya Mwaka B. (I. Hek 7:7-11; II. Ebr 4:12-13; III. Mk 10:17-30)
  • Sikukuu ya Komunyo ya Kwanza.
  • Siku hiyo ibada zitakuwa mbili.  Misa ya kwanza saa 12:30 asubuhi na Misa ya pili ni saa 3:30 kamili ambapo kwenye misa ya pili watoto watapokea Komunyo ya Kwanza.
  • Utegemezaji wa Kanisa, ni zamu ya Jumuiya ya Mt. Fransisko wa Asizi.

14-10-2015. Jumatano
  • Mafundisho kwa Wazazi na Wasimamizi wa watoto wa ubatizo, saa 11:00 jioni kwenye Kanisa dogo.  Wazazi / Walezi wote wawili wahakikishe wanahudhuria mafundisho hayo pamoja na wasimamizi.

17-10-2015. Jumamosi
  • Ubatizo wa Watoto wachanga saa 4:00 asubuhi.
  • Misa katika Jumuiya ya Mt. Veronika saa 12:30 asubuhi.

18-10-2015.  Dominika ya 29 ya Mwaka B. (I. Isa 53:10-11; II. Ebr 4:14-16; III. Mk 10:35-45)
  • Matoleo ya pili kwa ajili ya Misioni.

21-10-2015. Jumatano
  • Misa ya somo katika Jumuiya ya Mt. Yohani Paulo II. Saa 11:00 jioni.  Sikukuu yake huadhimishwa kila tarehe 22 –Oktoba. 

23-10-2015. Ijumaa
  • Novena kwa ajili ya maandalizi ya kiroho kwa wanafunzi wa Kipaimara.  Novena itakuwa ikisaliwa kwenye familia za wanafunzi wa Kipaimara.
  • Kikao cha Kamati Tendaji saa 11:30 jioni kwenye Ofisi ya Parokia.

24-10-2015. Jumamosi
  • Misa ya Mtaa – Mtaa wa Bethania; saa 12:30 asubuhi.

25-10-2015. Dominika ya 30 ya Mwaka B. (I. Yer. 31:7-9; II. Ebr.5:1-6; III. Mk. 10:46-52)
  • Matoleo ya pili kwa ajili ya Seminari.
  • Utegemezaji wa Kanisa, ni zamu ya Jumuiya ya Mt. Yohani Mbatizaji.
·         Ibada ya Matamanio ya kumpokea ROHO MTAKATIFU kwa wanafunzi wa Kipaimara.
  • Maandamano kwa Heshima ya Mama Bikira Maria. 
·         Siku hiyo Misa itakuwa moja itakayoanza saa 1 : 00 asubuhi.    Maandamano hayo yatakuwa na vituo vitatu.  Kituo cha kwanza ni Kitongoji cha Sabore Kituo cha pili ni Ofisi ya Kijiji, Kituo cha tatu ni Kanisani. Jumuiya za MtaawaYerusalemu watahusika kwa upambaji wa Kituo cha Kwanza (Kitongoji cha Sabore).  Jumuiya za MtaawaNazareti zitahusika kwa upambaji wa Kituo cha Pili (Ofisi ya Kijiji).
  • Dominika ya kuwasilisha michango ya Usafi wa Kanisa toka kila Jumuiya shilingi 15,000/=.

26-10-2015. Jumatatu
  • Misa na Neno la Kiroho kwa wanakwaya wa Kwaya zote saa 11:00 jioni.

27-10-2015. Jumanne
  • Maungamo kwa Watoto wanaojiandaa kupokea Sakramenti ya Kipaimara pamoja na Wazazi na Walezi wao.  Maungamo yataanza saa 9:00 alasiri.

28-10-2015. Jumatano
  • Sikukuu ya Somo wa Jumuiya ya Mt. Yuda Tadei.  Misa saa 11:00 Jioni.

30-10-2015. Ijumaa
  • Ibada ya Misa ya kubariki mavazi ya watoto watakaopokea Sakramenti ya Kipaimara.  Ibada itaanza saa 11:00 jioni.

31-10-2015. Jumamosi
  • Misa katika Jumuiya ya Mt. Sesilia saa 12:30 asubuhi.

NOVEMBA

Mwezi Novemba ni mwezi ambao Mama Kanisa anawaalika waamini kuwaombea marehemu walioko Toharani.  Waamini wanaalikwa kuomba misa kwa aajili ya kuwaombea marehemu wetu.  Kutembelea Makaburi kwa uchaji au kuwaombea kupata rehema kamili kwa ajili ya marehemu siku nane za kwanza mwezi Novemba.  Siku nyingine za mwaka ni kupata rehema za muda.

01-11-2015. Dominika ya Watakatifu wote. (I. Ufu 7:2-4, 9-14; II. 1Yo 3:1-3; III. Mt 5:-12)
  • Mkutano wa Halmashauri Parokia mara tu baada ya misa ya kwanza.
  • Sikukuu ya Kipaimara.
  • Misa zitakuwa mbili.  Misa ya Kwanza saa 12:30 na Misa ya pili saa 3:30, misa ambayo watoto watapokea Sakramenti ya Kipaimara.

02-11-2015. Jumatatu; KUWAKUMBUKA MAREHEMU WOTE
  • Misa zitakuwa tatu.  Misa ya kwanza, saa 12:30 asubuhi.  Misa ya pili, saa 6 :30 mchana na Misa ya tatu saa 11 :00 jioni. 

04-11-2015. Jumatano
  • Misa katika Jumuiya ya Mt. Teresia wa Mtoto YESU saa 12:30 asubuhi.

05-11-2015. Alhamisi ya kwanza ya mwezi
  • Kuabudu Ekaristi Takatifu kwa kimya kuanzia saa 1: 00 asubuhi mara tu baada ya misa na kuhitimishwa kwa Masifu ya Jioni na Baraka ya Sakramenti Kuu saa 11:00 kamili.

07-11-2015. Jumamosi
  • Misa ya Mtaa – Mtaa wa Galilaya; saa 12:30 asubuhi.

08-11-2015. Dominika ya 32 ya Mwaka B. (I. 1Fal 17:10-16; II. Ebr 9:24-28; III. Mk 12:38-44)
·      Matoleo ya Pili kwa ajili ya Symposium of Episcopal Conferences of Africa and Madagascar (SECAM – Umoja wa Mabaraza ya Maaskofu Afrika Masharini na   ya Kati na Madagaska).
  • Utegemezaji wa Kanisa, ni zamu ya Jumuiya ya Mt. Klara wa Asizi.

14-11-2015. Jumamosi
  • Misa katika Jumuiya ya Wat. Malaika wakuu saa 12:30 asubuhi.

15-11-2015. Dominika ya 33 ya Mwaka B. (I. Dan 12:1-3; II Ebr 10:11-14,18; III. Mk 13:24-32)
  • Matoleo ya pili kwa ajili ya Seminari.
  • Uhamasishaji wa Sikukuu ya Mavuno / shukrani na Somo wa Parokia.

19-12-2015. Jumatano
  • Misa katika Jumuiya ya Mt. Yosefina Bakita saa 12:30 asubuhi.

20-11-2015. Ijumaa
  • Mkesha Mtakatifu wa Kuabudu Ekaristi Takatifu pamoja na Neno la Kiroho na Sakramenti ya Upatanisho. Mkesha utaanza saa 3:00 usiku na kuhitimishwa kwa Ibada ya Misa Takatifu saa 12:00 asubuhi.  Waamini tujitokeze kwa wingi.

21-11-2015. Jumamosi
  • Sikukuu ya Somo wa Jumuiya ya Mt. Sesilia.  Misa saa 12:30 asubuhi.

22-11-2015. YESU KRISTO Mfalme. (I. Dan 7:13-14; : II. Ufu 1:5-8; III. Yn 18:33-37)
·         Uhamasishaji juu ya Sikukuu ya Shukrani.

27-11-2015. Ijumaa
  • Mwanzo wa Novena kwa ajili ya kujiandaa na Sikukuu ya Somo wa Parokia na siku ya Mavuno.  Novena itakuwa ikisaliwa kwenye Jumuiya kwa siku 9.  Viongozi wa Kamati Tendaji, na Kamati ya Fedha uchumi na Mipango watagawanywa kwenye Jumuiya ili kushiriki Novena hiyo na Jumuiya nyingine na kuwahamasisha.
  • Kikao cha Kamati Tendaji saa 11:30 jioni kwenye Ofisi ya Parokia.

28-11-2015. Jumamosi
  • Misa ya Mtaa – Mtaa wa Nazareti; saa 12:30 asubuhi.

29-11-2015. Dominika ya 1 ya Majilio Mwaka C. (I. Yer 33:14-16; II. 1Thes 3:12-4:2; III. Lk. 21:25-28,34-36)
  • Sadaka ya pli wa ajili ya Seminari.
  • Utegemezaji wa Kanisa, ni zamu ya Jumuiya ya Mt. Monika.
  • Uhamasishaji juu ya Sikukuu ya Somo na Mavuno.
  • Dominika ya kuwasilisha michango ya Usafi wa Kanisa toka kila Jumuiya shilingi 15,000/=.

30-11-2015. Jumatatu
  • Misa na Neno la Kiroho kwa wanakwaya wa Kwaya zote saa 11:00 jioni.

DESEMBA

02-11-2015. Jumatano
MAUNGAMO KWA AJILI YA KUJIANDAA NA SIKUKUU YA SOMO WA PAROKIA NA MAVUNO. 

04-12-2015. Ijumaa
  • Maungamo kwa watu wazima yataanza saa 11:00 kamili jioni.

05-12-2015. Jumamosi
  • Misa ya Somo ya Jumuiya katika Jumuiya ya Mt. Baltazari saa 11:00 jioni.
  • Maungamo kwa watoto yataanza saa 3:00 kamili asubuhi.

06-12-2015. Dominika ya 2 ya Majilio Mwaka C. (I. Bar 5:1-9; Flp 1:4-6,8-11; III. Lk 3:1-6)
  • Sikukuu ya Somo wa Parokia.
  • Misa ni moja saa 3:00 asubuhi.
  • Maonesho ya Vibanda kwa vyama vya kitume na Kwaya.
  • Waamini wataandamana toka katika Mitaa yao na kupokelewa na Paroko kwenye Mlango mkubwa wa Parokia.
  • Siku ya kila Jumuiya kuwasilisha Sadaka yao ya Mavuno / Shukrani ya Mwaka.
  • Siku ya kutoa zawadi kwa washindi mbalimbali kutokana na michezo iliyoshindaniwa kwa ajili ya Maadhimisho ya Sikukuu ya Somo wa Parokia.

12-12-2015. Jumamosi
  • Misa ya Mtaa – Mtaa wa Bethlehemu; saa 12:30 asubuhi.

13-12-2015. Dominika ya 3 ya Majili Mwaka C. (I. Sef 3:14-18; II. Flp 4:4-7; III. Lk 3:10-18)

14-12-2015. Jumatatu
  • Ibada ya baraka maalum kwa kina mama wote wajawazito.  Baraka hiyo itatolewa saa 11:00 jioni hapa kanisani.  Kina mama wote wajawazito wafike kwenye ibada hiyo kwa nia ya kuwabariki na kumwomba.

18-12-2015. Ijumaa
  • Kikao cha Kamati Tendaji saa 11:30 jioni kwenye Ofisi ya Parokia.

20-12-2015. Dominika ya 4 ya Majili Mwaka C. (I. Mik 5:2-4; II. Ebr 10:5-10; III. Lk 1:39-45)
·         Matoleo ya Pili kwa ajili ya Nchi Takatifu (OMNIA TERRA).
  • Utegemezaji wa Kanisa, ni zamu ya Jumuiya ya Mt. Agustino.

22-12-2015. Jumanne
  • Mafundisho kwa Wazazi na Wasimamizi wa watoto wa ubatizo, saa 11:00 jioni kwenye Kanisa dogo.  Wazazi / Walezi wote wawili wahakikishe wanahudhuria mafundisho hayo pamoja na wasimamizi.

24-12-2015. Jumatatu
·         Misa ya Mkesha wa Sikukuu ya Kuzaliwa kwake BWANA wetu YESU KRISTO itaanza saa 2.00 usiku.
·         Ndoa za jumla kwenye mkesha wa Noeli.

25-12-2015. Ijumaa, Kuzaliwa kwake YESU KRISTO. (I. Isa 52:7-10; II. Ebr 1:1-6; III. Yn 1:1-18)
·         Misa zitakuwa mbili.  Misa ya kwanza saa 12:30 asubuhi na Misa ya pili saa 3:00 asubuhi.

26-12-2015.Jumamosi- Sikukuu ya Mt. Stefano, Shahidi, . (I. Mdo. 6:8-10; 7:54-60; Mt. 10:17-22) 
  • Misa itakuwa moja na itaanza saa 1 :00 asubuhi.
  • Ubatizo wa Watoto wachanga.

27-12-2015. Sikukuu ya Familia Takatifu. (I. YbS 3:2-6, 12-14; II. Kol 3:12 -21; III. Lk 2:41-52)
  • Siku rasmi kwa kila familia kutoa Matoleo maalumu ya kutegemeza Parokia kama sehemu ya kumshukuru MUNGU kwa maisha ya Familia.  Kila familia itapata nafasi ya kutoa Matoleo yao maalumu.
  • Baraka ya Familia itatolewa ili familia zote zibarikiwe.
  • Misa itakuwa moja itakayoanza saa moja asubuhi ili familia nzima ifike Kanisani na kukaa pamoja.
  • Sikukuu ya Utoto Mtakatifu.
  • Ibada ya kuwakaribisha na kuwapokea rasmi wageni wote waliohamia na kujiunga na Parokia yetu kuanzia mwezi wa Nane 2015.
  • Dominika ya kuwasilisha michango ya Usafi wa Kanisa toka kila Jumuiya shilingi 15,000/=.

28-12-2015. Jumatatu
  • Misa na Neno la Kiroho kwa wanakwaya wa Kwaya zote saa 11:00 jioni.

31-12-2015. Alamisi
  • Misa ya kufunga Mwaka 2015 itaanza saa 11:00 Jioni.  Waamini wote watakaoshiriki Ibada ya misa hiyo wafike na mishumaa.

**************************************************************

Semina za Kiroho kwa mwaka 2015

Tunatarajia kuwa na semina mbalimbali za kiroho kama ifuatavyo :-
  1. Seina ya uongozi kwa viongozi wote mara 3
  2. Semina ya ndoa mara 4
  3. Semina kwa vijana mara 4
  4. Semina kwa vyama vya kitume mara 3
  5. Semina kwa watoto mara 4
  6. Semina kwa waamini wote mara 3
Semina hizi zitapangiwa muda kadiri ya nafasi ya wawezeshaji itakavyokuwa ikipatikana.

Mikutano ya Kamati mbalimbali
Mikutano kwa Kamati Mbalimbali itapangwa na Kamati husika.  Tunashauri kila mwezi kuwepo na Mkutano mmoja kwa kila Kamati.  Kamati hizo ni :-

  1. Kamati ya Liturujia na Katekesi – Mwenyekiti ni Theodory Mosshy
  2. Kamati ya Haki na Amani –Mwenyekiti ni Mary-Goreth Temu
  3. Kamati ya Vjijana na Miito – Mwenyekiti ni Ibrahimu Julius Kayanda
  4. Kamati ya Fedha, Uchumi na Mipango – Mwenyekiti ni Dionise Moyo
  5. Shirikisho la Vyama vya Kitume – Mwenyekiti ni Raphael Temu
  6. Shirikisho la Kwaya – Mwenyekiti ni Stella Julian Mnyang’ali
  7. Kamati ya Wasiojiweza – Viongozi ni Donovan John Mwanga na Livingstone Mark Nguma.
  8. Kamati ya WAWATA – Mwenyekiti ni Veneranda StephenManjira
  9. Kamati ya Watoto – Viongozi ni Daria Abel na Katekista Edmund Mmassy

Sherehe za vyama vya kitume
Sherehe za Vyama vya Kitume na Kwaya zitapangwa kulingana na nafsi zao kwa kumshirikisha Paroko.

Ratiba ya saa za misa siku za wiki
Jumatatu hadi Ijumaa
Masifu ya asubuhi saa 12 :00 hadi saa 12 :25 asubuhi
Misa ya asubuhi saa 12 :30 asubuhi

Ratiba ya Saa za misa siku za Dominika
Misa ya kwanza saa 12 :30 hadi saa 2:00 asubuhi (Misa kwa ajili ya watu wazima)
Misa ya pili saa 2 :30 hadi saa 4 :00 asubuhi (Misa wa ajili ya vijana)
Misa ya pili  saa 4 :00 hadi saa 5 :30 asubuhi (Misa kwa ajili ya watoto)

Ratiba ya Maungamo
Jumamosi saa 1:00 hadi saa 2:30 asubuhi na wakati wowote pale mwamini anapokuwa anahitaji kupokea sakramenti hiyo.  Jioni saa 11 :00 hadi saa 12 :30
N.b.Sakramenti ya Kitubio yaweza kutolewa saa yeyote panapotokea hitaji.

Ratiba ya Mafundisho
Komunyo ya Kwanza na Kipaimara-
Jumamosi saa 2:00 asubuhi  hadi saa 6:00 mchana
Jumapili saa 8:00 mchana hadi saa 10:30 jioni

Ibada ya Baraka ya Sakramenti Kuu
Kila siku ya Alhamisi saa 11: 00 hadi saa 12:00 jioni ibada hiyo inaanza na Masifu ya Jioni.

Baraka mbalimbali zinazoweza kutolewa na Padre kwa waamini wanaohitaji :-
Baraka ya Familia. Baraka ya Watoto. Baraka ya Wachumba. Baraka ya Wazazi kabla ya Mtoto kuzaliwa. Baraka ya Mama kabla na baada ya mtoto kuzaliwa.  Baraka ya Mama ambaye mimba imetoka.  Baraka ya Wazazi wenye mtoto wa kumlea.  Baraka ya Siku ya kuzaliwa. Baraka ya Walimu na wanafunzi.  Baraka ya Wasafiri (Mtu anayetaka kusafiri). Baraka ya Eneo la ujenzi. Baraka ya Ofisi – Duka – Kiwanda. Baraka ya Vyombo vya usafiri. Baraka ya Vyombo vya Kazi. Baraka ya Wanyama. Baraka ya Mashamba. Baraka ya mbegu.

Vyama vya Kitume
Parokia ina vyama vya kitume vifuatavyo:
1.      Shirika la Mt. Yosefu
Wanachama wake hukutana kila Alhamisi mara tu baada ya ibada ya kuabudu Ekaristi Takatifu kwenye Kanisa dogo.

2.      Shirika la Kipapa.
(Utoto wa YESU).  Wanachama hukutana kila siku ya Ijumaa saa 10:00 jioni na Jumamosi saa 10:00 jioni kwenye kanisa dogo.

3.      VIWAWA
Wanachama wake hukutana kila Dominika mara tu baada ya misa ya Pili.

4.      WAWATA
Wanachama wake hukutana kila Dominika ya mwisho wa mwezi, katika kanisa dogo.

5.      Kwaya ya Mt. Kizito 
Wanakwaya hukutana kwa mazoezi kila siku za Jumanne, Alhamisi na Jumamosi.

6.      Kwaya ya Ekaristi Takatifu
Wanakwaya hukutana kwa mazoezi kila siku za Jumanne, Jumatano, Ijumaa na Jumamosi.

7.      Mt. Aloisi (Watumishi)
Wanachama wake hukutana kila siku ya Jumamosi kuanzia saa 8:00 mchana.

8.      Shirika la Rozari Takatifu
Wanachama wa Shirika la Rozari Takatifu hukutana kila siku ya Jumamosi kanisani kuanzia saa 10:30 hadi saa 11:00 jioni.

9.      Karismatiki Katoliki
Hukutana kila siku za Dominika na Jumatatu saa 10:00 hadi saa 12:30 jioni

KAMATI MBALIMBALI
  1. Kamati Tendaji
Inaundwa na:-
Paroko, Mwenyekiti wa Parokia, Makamu Mwenyekiti, Katibu, Katibu Msaidizi, Mweka hazina na (Mweka hazina Msaidizi).

  1. Baraza la kichungaji
Linaundwa na:-
Wajumbe wote wa Kamati Tendaji, Mwenyekiti na Katibu wa kila Mtaa, Mwenyekiti na Katibu wa kila Kamati ndogo ambazo ni:- Kamati ya Liturujia na Katekesi, Kamati ya Fedha na mipango, Kamati ya Watoto, Kamati ya Haki na Amani, Kamati ya WAWATA, Kamati ya Shirikisho la Kwaya, Kamati ya Shirikisho la Vyama vya Kitume, Kamati ya wasiojiweza, Kamati ya Vijana na Miito.

  1. Halmashauri ya Parokia
Inaundwa na:- Viongozi wote wa Jumuiya Ndogo Ndogo, Viongozi wote wa Vyama vya Kitume na wajumbe wa Kamati ya Fedha, uchumi na mipango.

  1. Viongozi wa Mitaa
Viongozi wote wa  Mtaa Mwenyekiti, Katibu na Mweka hazina.

MAJUKUMU YA KAMATI ZA MITAA / KATA NA KAMATI NDOGO NDOGO ZA PAROKIA
MAJUKUMU YA VIONGOZI WA MITAA / KATA

  1. Kuhimiza  uhai wa Jumuiya katika kipindi chote cha utendaji wao.
  2. Kuhakikisha  wajumbe wote 11 kwa kila Jumuiya wapo, na ikiwa pametokea upungufu wa mjumbe yeyote katika wale 11, watoe taarifa kwa Kamati Tendaji ya Parokia ili uchaguzi mdogo ufanyike mara moja.
  3. Waitishe vikao vya pamoja na hao wajumbe 11 wa kila Jumuiya.  Vikao hivyo viitishwe kila baada ya miezi mitatu ili kupata maendeleo ya Jumuiya hizo na kutoa taarifa yao kwa mikutano ya Kamati ya Utekelezaji ya Parokia ambayo inafanya vikao vyake kila baada ya miezi mitatu.
  4. Kutembelea Jumuiya zao mara kwa mara ili kujua matatizo yaliyopo Jumuiyani, na kujaribu kuyatatua.  Kama tatizo ni  kubwa kiasi cha kushindwa kulikabili, watoe taarifa kwa Kamati Tendaji ya Parokia kwa ufumbuzi zaidi.
  5. Kuhimiza  na kuhakikisha wajumbe wote 11 wanaonyesha mifano bora kwenye Jumuiya zao kwa mahudhurio mazuri katika siku maalum walizojipangia kusali.
  6. Wawe wafuatiliaji na wahamasishaji wa utoaji wa michango ya Kanisa, kama:- Zaka, Sadaka, Vipaji na michango mingineyo iliyopitishwa na kukubaliwa na Baraza la Parokia , kushiriki shughuli mbalimbali za Parokia n.k.
  7. Kuhakikisha na kufuatilia  suria na nyumba ndogo vinatoweka kabisa katika mitaa yao, tukianzia na Viongozi.
  8. Kuwahimiza na kuhakikisha viongozi 11 kwa kila Jumuiya  kwamba wanafanya vikao vyao kama ilivyoagizwa kwenye katiba.
  9. Kuhimiza Jumuiya  Ndogo Ndogo kutukuza somo wao kila mwaka kwa adhimisho la Misapamoja na somo wa Mtaa,  na ikiwezekana wafanye sherehe ndogo baada ya maandalizi ya kiroho kama vile kupokea Sakramenti ya Kitubio, au kufanya Novena n.k.
  10. Kuhudhuria vikao vya Baraza la Kicungaji / Halmashauri ya Utekelezaji Parokia.

MAJUKUMU YA KAMATI NDOGO NDOGO ZA PAROKIA

MAJUKUMU YA KAMATI YA LITURUJIA NA KATEKESI
  1. Kupanga na kusimamia shughuli na huduma mbali mbali Kanisani.
  2. Kuhakikisha kwamba Liturujia ya Kanisa kwa mwaka mzima inafuatwa.
  3. Kupendekeza na kuteua wasimamizi Kanisani.
  4. Kuthibiti nidhamu na kero zilizopo Kanisani.
  5. Kuratibu ufundishaji wa sala na ibada Kanisani.
  6. Kusimamia usafi na mapambo Kanisani (mazingira ya ndani na nje).
  7. Kuhakikisha kwamba Kwaya inawashirikisha waamini katika nyimbo za Liturujia.
  8. Kuweka ratiba muhimu za Ibada Kanisani.
  9. Kusimamia na kutunza vifaa vyote vya huduma Kanisani.
  10. Kuratibu na kusimamia mafundisho ya dini shuleni  na vyuo ambavyo viko katika eneo la Parokia.
  11. Kufanya vikao na Semina kuunganisha wawakilishi wa Liturujia na Katekesi kutoka Jumuiya Ndogo Ndogo.
  12. Ufundishaji wa Katekismu na sala Jumuiyani na kwa makundi mbali mbali kwa njia ya Semina.
  13. Kuratibu mafundisho endelevu ya waamini kuhusu Imani, kuanzia Jumuiyani hadi Parokiani.
  14. Kuandaa njia mbali mbali za kueneza Injili. Mfano:- Vipeperushi na michoro mbali mbali, makongamano na mafungo.
  15. Kuweka utaratibu wa Vikao vya Kamati ya Liturujia na Wasimamizi wa Kanisani.
  16. Kuhudhuria vikao vya Baraza la Kichungaji / Halmashauri ya Utekelezaji Parokia.
  17. Mfundisho ya ndoa na watumishi wa Misa.

MAJUKUMU YA KAMATI YA WATOTO
  1. Kuhakikisha watoto wanapatiwa mafundisho msingi ya Imani Katoliki.
  2. Kuratibu na kusimamia malezi ya watoto kuanzia Jumuiyani, hadi Parokiani.
  3. Kusaidiana na Viongozi wa Jumuiya Ndogo Ndogo kuwawezesha watoto kutambua miito yao.
  4. Kufanya vikao na Semina kuunganisha wawakilishi wa Watoto kutoka Jumuiya Ndogo Ndogo.
  5. Kubuni na kuandaa mafundisho, taratibu mbali mbali za michezo, burudani na vivutio mbali mbali kwa watoto vyenye mwelekeo wa kuwafundisha maadili.
  6. Kuhakikisha Watoto wanahudhuria Misa yao kadiri ya ratiba ya Kanisa.     
  7. Kuandaa vikao vya kamati ya Watoto
  8. Kuhudhuria vikao vya Baraza la Kichungaji / Halmashauri ya Utekelezaji Parokia.

MAJUKUMU YA KAMATI YA HAKI NA AMANI      
  1. Kuelimisha jamii  ya Parokia yetu kuhusu haki za raia.
  2. Kuhakikisha kuwa Haki na Amani inakuwepo katika familia, Jumuiya hadi Parokia.
  3. Kufanya vikao na Semina kuunganisha wawakilishi wa Haki na Amani kutoka Jumuiya Ndogo Ndogo.
  4. Kuunda Baraza la usuluhishi wa ndoa kulingana na mujibu wa sheria ya nchi.
  5. Kusuluhisha migogoro katika familia za Parokia yetu.
  6. Kubuni mbinu za kuwezesha Haki na Amani kupenyeza katika familia za Parokia yetu.
  7. Kuandaa vikao vya Kamati za Haki na Amani
  8. Kuhudhuria vikao vya Baraza la Kichungaji / Halmashauri ya Utekelezaji Parokia.

MAJUKUMU YA KAMATI YA WAWATA
  1. Kuwasaidia kina mama kuelewa na kutekeleza Utume wao katika Kanisa.
  2. Kuwaelekeza kadiri ya mwongozo wa WAWATA Jimbo, kuelewa na kutimiza vema Katiba ya Wanawake Wakatoliki Tanzania.
  3. Kuwahimiza katika maendeleo yao ya kiroho na kimwili.
  4. Kuwaandalia ratiba ya shughuli za matendo ya huruma na maendeleo ya Kiuchumi.
  5. Kuwahimiza kushiriki utoaji na Hazina ya Mwanamke kwa ajili ya Utendaji na Uwajibikaji wa Utume wa Mwanamke Mkatoliki.
  6. Kuandaa vikao vya Kamati ya WAWATA.
  7. Kuwahimiza Wanawake wa Parokia kushiriki katika maazimio mbali mbali ya Kiparokia na Kijimbo.
  8. Kufanya vikao na Semina kuunganisha wawakilishi wa WAWATA kutoka Jumuiya Ndogo Ndogo.
  9. Kuwahimiza kushiriki mchango wa Kituo cha Malezi ya Vijana Jimboni.
  10. Kuandaa vikao vya wawakilishi na Kamati Tendaji ya WAWATA Kiparokia.
  11. Kushiriki vikao vinavyoandaliwa na WAWATA Jimbo Kuu.
  12. Kuhudhuria vikao vya Baraza la kichungaji / Halmashauri ya Utekelezaji Parokia.

MAJUKUMU YA KAMATI YA VIJANA NA MIITO
  1. Kuhimiza Vijana kujiunga katika vikundi vya vijana. Parokiani, ambavyo ni Mt. Aloyce na VIWAWA.
  2. Kuratibu Semina mbali mbali za kuwasaidia Vijana kuelewa nafasi yao katika Kanisa na hatima ya miito yao.
  3. Kuandaa matamasha, makongamano na mafungo na mengineyo kwa ajili ya Vijana.
  4. Kufanya vikao na Semina kuunganisha wawakilishi wa Vijana na Miito kutoka Jumuiya Ndogo Ndogo.
  5. Kuandaa vikao mbali mbali vya Vijana Parokiani.
  6. Kuhudhuria vikao vya Halmashauri ya Utekelezaji Parokia.

MAJUKUMU YA KAMATI YA FEDHA, UCHUMI NA MIPANGO
  1. Kuweka kumbukumbu zote za mali na fedha za Parokia.
  2. Kusimamia miradi yote ya Parokia (kama ipo)
  3. Kubuni njia mbalimbali zinazotekelezeka za kuinua uchumi wa Parokia.
  4. Kuandaa bajeti ya Parokia na kuwakilisha kwenye Kamati Tendaji ya Parokia.
  5. Kutengeneza makisio ya mapato na matumizi ya Parokia kila mwaka.
  6. Kutengeneza taarifa ya mapato na matumizi kila mwezi na kuiwasilisha kwa Kamati Tendaji.
  7. Kufanya vikao na Semina kuunganisha wawakilishi wa Watunza Hazina  kutoka Jumuiya Ndogo Ndogo.
  8. Kushughulikia maslahi yote ya Parokia kwa Wafanyakazi. (ajira, nidhamu, mishahara, likizo n.k.).
  9. Kudhibiti matumizi ya fedha na mali ya Parokia na  Kuandaa vikao vya Kamati ya Fedha Uchumi na Mipango
  10. Kuhudhuria vikao vya Baraza la Kichungaji / Halmashauri ya Utekelezaji Parokia pamoja na Halmashauri ya Parokia.

MAJUKUMU YA KAMATI YA  WASIOJIWEZA
  1. Kutambua vitengo vinavyohusika na wasiojiweza katika Parokia yetu.
  2. Kutambua vyanzo vya fedha na misaada kwa ajili ya kusaidia wenye shida Parokiani.
  3. Kubuni mbinu za kuanzisha mfuko wa wasiojiweza Parokiani.
  4. Kufanya vikao na Semina kuunganisha wawakilishi wa wasiojiweza kutoka Jumuiya Ndogo Ndogo.
  5. Kuweka mfumo au utaratibu mzuri wa kuhudumia wenye shida.
  6. Kubuni siku moja katika mwaka kwa ajili ya sikukuu ya Wasiojiweza.
  7. Kuandaa Vikao vya Kamati ya wasiojiweza.
  8. Kuandaa na kusimamia maadhimisho ya sikukuu ya wasiojiweza - Siku ya Huruma ya MUNGU – kila mwaka.
  9. Kuhudhuria vikao vya Halmashauri ya Utekelezaji Parokia.

MAJUKUMU YA SHIRIKISHO LA KWAYA
  1. Kuandaa mikutano, semina na mafungo kwa ajili ya Kwaya zote ili kudumisha upendo, haki na amani kati yao.
  2. Kuhimiza Kwaya zote kujituma vilivyo katika kazi ya uenezaji Injili kwa njia ya nyimbo wakati wowote na mahali popote pindi watakiwapo kufanya hivyo.
  3. Kuhimiza Kwaya zote ziwe na Akaunti benki na kushughulikia vilivyo mapato na matumizi yao.
  4. Kuhimiza Kwaya zote kuwa na ratiba ya vikao kwa ajili ya maendeleo na majukumu yao ya kila siku.
  5. Kubuni mbinu mbali mbali za Kiuchumi za kuboresha Kwaya na Shirikisho pia.
  6. Kuhakikisha nyimbo za kwenye Ibada za Misa zinafuata Liturujia.
  7. Kutunza nidhamu pindi wawapo nje ya Parokia kiutume.
  8. Kuandaa Vikao vya Shirikisho la Kwaya.
  9. Kuhudhuria vikao vya Baraza la Kichungaji / Halmashauri ya Utekelezaji Parokia

MAJUKUMU YA KAMATI YA SHIRIKISHO LA VYAMA VYA KITUME PAROKIANI
  1. Kuhimiza kila chama kiwe na Katiba yake na kila mwanachama kupata nakala ili aisome, aielewe na kuitekeleza.
  2. Kuandaa Semina, makongamano au warsha mbali mbali za Shirikisho.
  3. Kuhimiza kila Chama au Shirika linaadhimisha sikukuu ya somo wao kwa Misa Takatifu kila mwaka baada ya maandalizi ya kiroho kama vile semina, mafungo na kupokea Sakramenti ya Kitubio.
  4. Kubuni mbinu mbali mbali za kiuchumi ili kuboresha utendaji wa Vyama na Shirikisho pia.
  5. Kuandaa utaratibu wa vikao vya Shirikisho la Vyama vya Kitume.
  6. Kuhudhuria vikao vya Halmashauri ya / Baraza la Kichungaji / Utekelezaji Parokia.

Post a Comment

Top