Hakuna familia ya wakamilifu. Hakuna wazazi wakamilifu, sisi siyo wakamilifu, hatufungi ndoa na wenza wakamilifu, na wala hatujazaa watoto wakamilifu.

Tunamalalamiko kadha wa kadha miongoni mwetu. Tunasononeshana hapa na pale. Kwahiyo hakuna ndoa au familia bora bila wajibu wa kusameheana.

Msamaha ni tiba muhimu kwa masononeko yetu na uhai wa roho zetu. Bila msamaha familia inakuwa ukumbi wa migogoro na taasisi ya kukuza chuki.
Bila msamaha familia inakuwa na maradhi. 

Msamaha husafisha roho na akili, na kuifungua mioyo yetu toka gerezani.
Yeyote asiyesamehe hakuna amani nafsini, wala hana ushirika na Mungu. 


Maumivu ni sumu inayoozesha na kuua. Kuhifadhi jeraha la moyo ni kitendo cha kujiangamiza mwenyewe. Ni kujiteketeza mwenyewe polepole.

Asiyesamehe anaugua kimwili, kihisia na kiroho. Ndiyo maana familia inapaswa kuwa mahali pa kuishi siyo mahali pa kufia; makao yaletayo uponyaji na siyo yaenezayo maradhi; na jukwaa la msamaha na siyo la hatia. 

Msamaha huleta furaha pale ambapo huzuni imeleta uchungu; na tiba pale ambapo uchungu umeleta maradhi. 

Have a blessed new year 2016.
Papa Fransis Vatican
25th.Dec.2015

Post a Comment

 
Top