REHEMA ni nini.

Rehema ni msamaha mbele ya Mungu wa adhabu ya muda kwa ajili ya dhambi ambazo kosa lao limekwishafutwa, msamaha ambao Mkristo mwamini aliyejiweka vizuri huupata kwa masharti  fulani yaliyopangwa kwa tendo la Kanisa ambao likawa mgawaji wa ukombozi hutumia mamlaka yake  hazina ya malipizi ya Kristo na ya Watakatifu.
Rehema inaweza kuwa ya muda au kamili kwamba yaondoa au sehemu  au adhabu yote kabisa ya muda inayotakiwa kwa sababu ya dhambi. Kila muumini anaweza kupata rehema kwa ajili yake au kwa ajili ya marehemu. (Rej. KWA 1471)
Katika mwaka huu huruma na rehema ya Mungu ni kwa wote wenye nia ya kuipokea rehema ya Mungu katika ukamilifu wake.
Kila mmoja akutane na uso wa huruma ya Mungu anayesamehe bila masharti.

Masharti ya kupata rehema kamili ni:-

πŸ‘‰πŸΏ  mhusika afanye hija katika mlango mtakatifu uliofunguliwa katika kila kathedrali au makanisa ya dekania yaliyoteuliwa kwa ajili ya hija. Kwenda huko ni kuonesha shauku ya WONGOFU
πŸ‘‰πŸΏrehema kamili inaweza kupatikana kwa kuhiji makanisa ya jubilei.
πŸ‘‰πŸΏ hata hivyo hija iambatanishwe na sakramenti ya upatanisho
🌟🌟🌟kuipokea Ekaristi Takatifu
🌟🌟🌟🌟🌟🌟kuikiri Imani
🌟🌟🌟🌟🌟🌟🌟🌟🌟 kusali kwa nia za Papa kwa ajili ya Kanisa

Kwa wagonjwa wasioweza kwenda katika hija itoshe kutafakari Fumbo la Pasaka, kushiriki adhimisho la Misa hata kupitia media hilo ni hitaji la kuwapatia rehema.

Post a Comment

 
Top