Neno “bikira” maana yake ni mwanamke ambaye hajaingiliwa na mwanaume.Hivyo Bikira Maria alibaki bikira kwa sababu hakuingiliwa na mwanaume yeyote katika maisha yake yote.Rejea Lk.1:34.
 Zaidi sana,Bikira Maria alipata mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu.Yaani,Roho Mtakatifu alifanyiza kutungika kwa mimba.Hata hivyo hii haimaanishi kuwa Roho Mtakatifu ndiye Baba yake Yesu au ndiye aliyerutubisha yai la Bikira Maria.Hivyo,utungwaji wa mimba wa Bwana wetu Kristo haukufanyika katika hali ya kawaida ya kibinadamu tuliyozoea.

Mtaguso Mkuu wa Laterano na Mtaguso Mkuu wa Trento inafundisha juu ya ubikira wa Mama Maria kabla ya kumzaa Yesu,wakati wa kumzaa Yesu na baada ya kumzaa Yesu.Mtaguso Mkuu wa pili wa Vatikano nao unafundisha juu ya ubikira wa mama Maria.Hii inapatikana katika sura ya nane (8) ya Mwanga wa Mataifa,namba 57,ambapo tunaambiwa, “Wakati wa kuzaliwa Bwana,Mwana hakuuondoa ubikira wa Mama yake bali aliutakatifuza.”Hivyo kanisa Katoliki linafundisha kuwa,Bikira Maria alikuwa bikira kabla ya kumzaa Yesu,wakati wa kumzaa Yesu na baada ya kumzaaYesu.Hivyo Maria ni bikira daima.

Katika mazungumzo kati ya Malaika na Maria,Malaika anamdokeza Maria kuwa hata baada ya kuchukua mimba,atabaki bikira,kwani mimba yake haitokani na mapenzi ya mwili bali ni kwa uwezo wa Roho Mtakatifu.
Mt.1:18-20.

Katika injili ya Marko (Mk.6:3) wanatajwa ndugu wake Yesu.Hawa si ndugu wa tumbo moja na Yesu,kama wengine wapatavyo utata.Hawa wanaotajwa hapa ni watoto wa Maria mke wa Kleopa.Wasemao kwamba,Bikira Maria alikuwa na watoto wengine baada ya Yesu,wanapata utata wasomapo Injili ya Mt.27:56 na Mk.15:40.Ukweli ni kwamba,Bikira Maria alikuwa bikira daima.Wala hakuwa na watoto wengine baada ya Yesu.

Pia ukisoma Yn.7:3-4 wanaotajwa kuwa ni ndugu wa Yesu wanaonekana kuwa na umri mkubwa kuliko Yesu.Kwani,kadiri ya utamaduni wa Kiyahudi,mkubwa kiumri ndiye anayepaswa kumshauri mdogo na si vinginevyo..Hivyo,wanaotajwa hapa si watoto wa Maria mama wa Yesu,kwani Yesu ndiye kifungua mimba na mwana pekee wa Maria.

Vilevile,kitendo chaYesu kumkababidhi mama yake kwa mfuasi wake (Yohane),kinaonyesha kuwa Yesu alikuwa mwana pekee, na bikira Maria hakuwa na watoto wengine zaidi ya Yesu.Kwani,katika jamii za Kiyahudi,watoto walijali sana kuwatunza wazazi wao.Hivyo,wao wangekuwa ndugu wa tumbo moja na Yesu wasingekubali kumwacha mama yao mikononi mwa rafiki.

Post a Comment

 
Top